Mashindano ya Samia, Jumbe Holiday kupigwa Desemba 31

MASHINDANO ya Samia/Jumbe Holiday Bonanza yanatarajiwa kufanyika katika Desemba 31, 2024 katika Uwanja wa CCM Kambarage huku washindi mbalimbali wa michezo itakayochezwa na kushindanishwa kujinyakulia zawadi nono.
Mratibu wa bonanza hilo, Jackline Isaro amesema hayo leo Desemab 27, mbele ya waandishi wa habari na baadhi ya wanamichezo na viongozi wao huku akieleza lengo la bonanza hilo ni kukuza vibaji vya vijana na kuleta Mahusiano kipitia michezo.

Isaro amesema michezo hiyo itakuwa kwa watu wenye umri wowote wanaume na wanawake ambapo hivi sasa baadhi ya Majaji wako mitaani kuhamasisha michezo inayoshindaniwa.
“Kutakuwa na bingwa wa wilaya Rangers na Ngokolo mshindi wa kwanza atapewa zawadi ya Sh 500,000 ng’ombe mmoja na kreti saba za soda na kilo 100 za mchele na mshindi wa pili Sh 300,000,kilo 100 za mchele na ng’ombe mmoja,”amesema Isaro.

Isaro amesema kutakuwa na mbio za baiskeli na washindi watakuwa wamegawanyika sehemu nne mshindi wa kwanzs hadi wa 10 atapata Sh milioni 2.1 mshindi mchezo wa bao, mchezo wa drafti,mchezo wa karata, msusi mwenye kasi zaidi wote watapata 100,000.
“Mchezo wa netboli au pete, mshindi wa kwanza na wa pili watapata shilingi 500,000,kreti saba za soda,mchele kilo 50, mshindi wa pili Sh 300,000 na mchele kilo 50 na kreti saba za soda,”amesema isaro.

Isaro amesema kutakuwa na mchezo wa mpira wa miguu kati ya upongoji derby ambazo timu hizo ni upongoji sports club na upongoji stars ikiwa mshindi wa atapewa zawadi ya Sh milioni moja, ngombe mmoja,mchele kilo 100 na kreti moja la soda.

Pia Isaro amesema mchezo wa kufukuza kuku,kula kwa wanaume na wanawake washindi watapata 20,000 pia mchezo wa pool table mshindi wa kwanza S 100,000 na mshindi wa Pili 50,000
Isaro amesema kutakuwa na mashindano ya kucheza mziki, ikiwemo mashindano ya Mpira wa miguu kati ya bodaboda na Bajaji na Mshindi wa kwanza shilingi 500,000 ngombe mmoja Kreti za Soda saba na kilo za mchele 100,000 Mshindi wa pili.




