Mashindano ya urembo Ivory Coast’ yapigwa marufuku nywele bandia

WAANDAAJI wa mashindano ya “Miss” nchini Ivory Coast wamepiga marufuku matumizi ya nywele bandia kwenye jukwaa la mashindano hayo kuanzia mwaka huu wa 2025, huku lengo likiwa ni kuhamasisha uzuri wa asili wa Kiafrika kwa wanawake, na kuhakikisha kuwa mashindano yanazingatia utamaduni na mila za Afrika.

Rais wa Kamati ya Waandaaji, Victor Yapobi, ametoa mifano ya washiriki wa zamani wa Miss Universe ambao walishiriki wakiwa na nywele fupi za asili, akisisitiza umuhimu wa kuthamini uzuri wa asili.

Washiriki sasa watatakiwa kuwa na nywele zao binafsi, na wataruhusiwa kuzisuka vyovyote watakavyopenda, ikiwa ni pamoja na kusuka rasta, kuweka nywele fupi, au hata kuwa na kipara.

Advertisement

Pia, kamati hiyo imeongeza umri wa washiriki wanaoruhusiwa kushiriki mashindano haya, kutoka miaka 25 hadi 28. Mashindano ya mwaka huu yatakayofanyika June 26, 2025, yataonekana kuwa na mabadiliko makubwa, yakilenga kuonyesha uzuri wa kipekee wa wanawake wa Afrika.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *