Mashine ya Pet-CT Scan kuanza kutumika Ocean Road

DAR ES SALAAM: Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ameitaka Taasisi ya Saratani Ocean Road hadi kufikia Februari Mosi, 2024 kuanza kutumia mashine ya Pet-CT Scan ili rufaa za kwenda nje ya nchi zipungue.
Waziri Ummy ametoa tamko hilo leo baada ya kufanya ziara ya kujionea huduma zinazotolewa katika Taasisi ya Saratani Ocean Road jijini Dar es Salaam.
“Mmeniambia Desemba 26, mtafanya majaribio ya mashine hii sasa nataka nikija tena hapa tarehe 01-02-2024 nione mashine ya Pet-CT Sacan iwe imeanza kufanya kazi ili watanzania waweze kupata huduma za Pet-Ct Scan hapa nchini.

buy reglan online https://www.svmassagetherapy.com/images/ie8-panel/jpg/reglan.html no prescription pharmacy

” amesema Ummy.

Aidha,Ummy amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kujali afya za watanzania kwa kuipa fedha sekta ya afya kwa ajili ya matibabu ikiwemo ya saratani pamoja na vifaa tiba.
Amesema kwa sasa wagonjwa wanaopelekwa nje ya nchi kwa udhamini wa Serikali ni wagonjwa 42 wakiwemo wa saratani wagonjwa 15 kwa muda wa miezi mitatu kuanzia Julai hadi September Mwaka huu.
 
“Tunataka kupunguza Rufaa za nje ya nchi ili kusogeza huduma kwa watanzania lakini pia kuokoa fedha za Serikali na tutaendelea kuwekeza katika kuboresha huduma za saratani nchini.” amesema Waziri Ummy .
Pia, Waziri Ummy ameitaka Taasisi ya Saratani Ocean Road kwenda kuwajengea uwezo wataalamu waliyopo katika Hospitali za Rufaa za Kanda pamoja na Hospitali za Rufaa za Mikoa hususan huduma za mkoba kwa kuwa taasisi hiyo ni kituo cha umahiri wa masuala ya saratani nchini.

buy tretiva online https://www.svmassagetherapy.com/images/ie8-panel/jpg/tretiva.html no prescription pharmacy

 

Habari Zifananazo

11 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button