Mashirika ya umma yamilikia ardhi bila hatimiliki

DODOMA — Ukaguzi wa mali za mashirika ya umma umebaini kuwa mashirika 18 yanamiliki viwanja 259 vyenye thamani ya Sh bilioni 201.67 bila kuwa na hatimiliki, kinyume na agizo la Wizara ya Ardhi la mwaka 2014.
Kukosekana kwa hati kunahatarisha umiliki wa mali hizo, hususan wakati wa migogoro ya kisheria au uvamizi. Sababu kubwa za hali hii ni ucheleweshaji wa mashirika kuomba hati na uwepo wa migogoro kwenye baadhi ya maeneo.
Ripoti ya CAG iliyotolewa leo imeorodhesha mashirika hayo kuwa ni pamoja na:
1. Shirika la Nyumba la Taifa – viwanja 139, sh. bil. 172.75
2. Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro – kiwanja 1, sh. bil. 8.00
3. Mamlaka ya Bandari Tanzania – viwanja 15, sh. bil. 7.62
4. Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara – viwanja 7, sh. bil. 2.51
5. Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo – kiwanja 1, sh. bil. 2.24
6. Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo – viwanja 15, sh. bil. 2.12
7. Kampuni ya Uendelezaji wa Jotoardhi – viwanja 2, sh. bil. 1.86
8. Mamlaka ya Majisafi Mwanza – viwanja 29, sh. bil. 1.70
(mashirika mengine 10 yenye jumla ya viwanja 49 vilivyosalia).
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu amependekeza mashirika yaweke kipaumbele kwenye kupata hatimiliki na kulinda ardhi dhidi ya uvamizi.



