Masomo ya sayansi, teknolojia kuongeza ujuzi wa wanafunzi

ARUSHA: UFUNDISHAJI wa masomo ya sayansi, teknolojia,uhandisi na hisabati (STEM) yanawezesha wanafunzi kupata ujuzi na maarifa yanayosaidia kujitegemea ikiwemo kutatua changamoto za jamii zinazozunguuka
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari ya Tumaini Senior ,Modest Bayo katika mahafali ya kidato cha sita ambapo jumla ya wanafunzi 56 walimaliza shule katika fani mbalimbali ya sayansi na masomo mengine.
Amesema masomo hayo yanasaidia wanafunzi katika ujifunzaji kwa vitendo kupitia teknolojia mbalimbali ili kujikwamua kimasomo zaidi
Ametoa rai kwa wanafunzi hao kusoma kwa bidii na kujilinda na magonjwa mbalimbali na kutokubali kurubuniwa na watu wasio na nia njema kwani serikali na wazazi wamewekeza katika elimu hivyo wahakikishe wanatumia ujuzi waliopata kujikwamua kimaisha
Naye Mkuu wa shule hiyo, Sifael Msengi amesema shule hiyo inatoa mafunzo ya sayansi jamii , biashara na masomo mengine kwani wamekuwa wakifanya vema huku akisisitiza ushirikiano mzuri kati ya wazazi, walezi, walimu pamoja na wanafunzi kwa kuweka mikakati ya kufanya mitihani kwa wingi ya ndani na nje ikiwemo kumaliza topiki za masomo kwa wakati



