Mataifa 54 yaunga mkono agenda nishati safi

AGENDA ya Nishati safi ya kupikia iliyoanzishwa na Rais Samia Suluhu Hassan imeungwa mkono ni nchi 54 za Afrika na ikitajwa kuwa ni miongoni mwa vipaumbele vikuu vitakavyoiwakilisha Afrika kwenye Mkutano wa 30 wa Mabadiliko ya Tabia Nchi (COP30) unaotarajia kufanyia kuanzia Novemba 6 mwaka huu nchini Brazil.

Hali hiyo imeonyesha kuwa Tanzania imeendelea kuwa na uongozi thabiti chini ya Rais Samia Suluhu Hassan katika juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ili jamii iweze kuondoka katika kupika kwa kutumia kuni.

Akizungumza jijini Arusha leo katika kikao cha maandalizi kilichokutanisha wataalam wa mabadiliko ya tabianchi kutoka nchi 54 za Afrika, Mwenyekiti wa kundi la Afrika la wataalam wa mabadiliko ya tabianchi (African Group of Negotiators – AGN), Dkt Richard Muyungi, alisema Afrika imekubaliana kwa pamoja kubeba ajenda hiyo kama moja ya nguzo kuu za majadiliano yatakayofanyika Belem, Brazil.

Dk Muyungi, ambaye pia ni mshauri wa Rais Samia Suluhu Hassan katika masuala ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi, alisema ajenda ya nishati safi ya kupikia inalenga kubadilisha maisha ya mamilioni ya wananchi barani Afrika kwa kuondoa utegemezi wa nishati chafu na kupunguza uharibifu wa mazingira.

“Rais Dk Samia Suluhu Hassan amekuwa kinara wa ajenda ya nishati safi ya kupikia, na kama Afrika tumeamua kuibeba kwa nguvu moja. Ni ajenda inayogusa afya, uchumi na ustawi wa jamii, hivyo lazima tuipeleke Brazil tukiwa na msimamo wa pamoja,” alisema Dk Muyungi.

Kwa mujibu wa Dk Muyungi, mkutano huo pia utajadili utekelezaji wa makubaliano ya Paris, hususan kifungu cha 6 cha sheria{Article 6}, ambayo inahusu mifumo ya kibiashara ya kaboni na ushirikiano wa kimataifa katika kupunguza hewa ukaa.

Akifafanua zaidi, Afisa Mazingira Mwandamizi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Makuru Nyarobi, alisema kikao hicho kimekuwa sehemu ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalam wa Afrika ili waweze kushiriki majadiliano kwa sauti moja na kwa uelewa wa pamoja.

Kwa upande wake, Mwenyekiti mstaafu wa AGN, Dk Alick Muvundika, alisisitiza kuwa Afrika ina wajibu wa kutumia majadiliano hayo kuendeleza vipaumbele vyake vya maendeleo endelevu, ikiwemo kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2030, takribani Waafrika milioni 300 wanakuwa wamepata nishati ya umeme.

Naye Ofisa Mwandamizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), Frida Mwakasuka, alisema UNDP itaendelea kushirikiana na serikali za Afrika katika kutoa rasilimali, teknolojia na utaalamu utakaosaidia utekelezaji wa ajenda hizo.

Kwa ujumla, washiriki wa kikao hicho wamekubaliana kwamba bara la Afrika linapaswa kuingia kwenye majadiliano ya Brazil likiwa na msimamo mmoja, unaojikita katika kutumia mabadiliko ya tabianchi kama fursa ya maendeleo badala ya changamoto.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..

    .

    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button