Mati Super Brands wajiandisha kupiga kura

MKURUGENZI Mtendaji wa Kampuni ya kuzalisha vinywaji changamshi ya Mati Super Brands Limited, David Mulokozi ameongoza wafanyakazi wa kampuni hiyo kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga kura katika kituo cha Bagara Sekondari  wilayani Babati mkoani Manyara leo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kuzalisha vinywaji changamshi ya Mati Super Brands Limited ya Mkoani Manyara, David Mulokozi (Kulia) akijiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga kura katika Kituo Cha Bagara Sekondari wilayani Babati mkoani Manyara leo (Picha na Mpiga Picha Wetu)

Mulokozi amesema zoezi hilo linafanyika kwa utaratibu mzuri ambao unamuwezesha kila mwananchi kujiandikisha kwa urahisi na kuendelea na shughuli za uzalishaji mali bila kuathiri ratiba zao za kila siku.

“Leo nimetimiza haki yangu ya kujiandikisha ili niweze kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu, na Uchaguzi Mkuu mwakani, nimechukua dakika chache kuboresha taarifa zangu kwa kuwa nilishawahi kujiandikisha, hivyo nilikua nahamisha taarifa zangu kuja hapa ninapoishi kwa sasa,” alisema Mulokozi.

SOMA: Mulokozi kuzindua mradi mpya wa elimu

Mulokozi ametoa wito kwa vijana na wakazi wa Mkoa wa Manyara kujitokeza kwa wingi kujindikisha kwani zoezi hilo halichukui muda mrefu na hakuna foleni.

Habari Zifananazo

Back to top button