Teknolojia Ai izingatie maadili na tamaduni

DAR-ES-SALAAM: MWAKILISHI kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Lilian Shirima, amesema serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya kidigitali ili kuhakikisha Tanzania inafuatilia mabadiliko ya teknolojia yanayoendelea duniani.

Akifungua hafla ya uwasilishaji wa ripoti ya utafiti kuhusu matumizi ya teknolojia ya akili mnemba (AI) kwa maendeleo ya vyombo vya habari, uliofanywa na Shirika lisilo la kiserikali linaloshughulikia maendeleo ya ICT (TMC),

Lilian amesema  kuwa serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuunda mifumo itakayodhibiti viwango vya maadili, kuhakikisha kuwa manufaa ya ubunifu wa teknolojia ya AI yanakuwa salama kwa maslahi ya Watanzania.

“Tumejizatiti kusaidia juhudi zinazolenga kuunda suluhisho za AI zinazozingatia muktadha wetu wa lugha na tamaduni za Tanzania,” alisema Lilian.

SOMA:Viongozi, wadau wa Tehama msiogope teknolojia ya AI

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button