Viongozi, wadau wa Tehama msiogope teknolojia ya AI

MAREKANI : MAKAMU wa Rais wa Marekani, J.D. Vance, amewaondoa hofu viongozi duniani na wadau wengine wa teknolojia ya akili mnemba na kusisitiza kuwa mabadiliko ya teknolojia yanaweza kuleta matumaini mapya katika harakati za ukuaji wa uchumi duniani.

Akizungumza Jumanne mjini Paris katika mkutano wa kilele kuhusu akili mnemba, kwa niaba ya Rais Donald Trump, Vance alisema kuwa Marekani inatambua umuhimu wa teknolojia hii ni muhimu kuwa na uangalizi ili zisizodhoofishe maendeleo ya teknolojia.

Vance aliongeza kuwa kuweka kanuni kali kunaweza kukadumaza maendeleo ya teknolojia ya akili mnemba na ubinifu wake .SOMA: Samsung kuimarisha ubunifu akili mnemba na matumizi ya kidijitali Tanzania

Advertisement

Alisisitiza kwamba dunia sasa ipo katika mapinduzi mapya ya viwanda, ambayo yanahitaji teknolojia za kisasa ili kuharakisha maendeleo ya uchumi duniani.

SOMA:

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *