Wajumbe wa Iran, Marekani wakutana na PM Pakistan

ISLAMABAD, Pakistan — Ujumbe wa Iran umefanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Pakistan, Shehbaz Sharif, jijini Islamabad, huku pia Makamu wa Rais wa Marekani, JD Vance, akiendelea na mazungumzo yake na kiongozi huyo, kwa mujibu wa Ikulu ya Marekani.

Ujumbe wa Iran unaongozwa na Spika wa Bunge Mohammad Bagher Qalibaf na unamjumuisha Waziri wa Mambo ya Nje Abbas Araghchi.

Maelezo ya kina ya mazungumzo hayo bado hayajatolewa, huku yakitarajiwa kuathiri mwelekeo wa juhudi za kusitisha vita vinavyoendelea kati ya Marekani na Iran.

Wakati huo huo, kundi la Hamas limeunga mkono mazungumzo hayo, likisema lina matumaini yatafanikisha kumaliza kabisa vita na kuimarisha utulivu wa kikanda.

Katika taarifa yake, Hamas imesisitiza umuhimu wa juhudi za Pakistan na nchi nyingine wapatanishi katika kuleta matokeo chanya yatakayochochea mshikamano miongoni mwa nchi za Kiarabu na Kiislamu.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…

    THIS→→→→ https://Www.FindJobs1.Site

  2. Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earnimng from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…

    THIS→→→→ https://Www.FindJobs1.Site

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button