Matumzi ya vilevi hatari ukomo wa hedhi

DAKTARI bingwa wa magonjwa ya uzazi na masuala ya wanawake Hospitali ya Taifa Muhimbili(MNH), Dk Lilian Mnabwiru amesema endapo mwanamke ambaye anakumbana na dalili za ukomo wa hedhi anapaswa kubadili mtindo wa maisha ikiwemo kuacha matumizi ya vilevi.

Akizungumza na Dailynews Digital  jijini Dar es Salaam ,Dk Lilian amesema vilevi wanavyotakiwa kuacha ni matumzi ya sigara, tumbaku ,cafen na vitu vyote vyenye cafen ikiwemo kahawa,energy drinks na kupunguza matumizi ya sukari na chumvi

“Wafanye mabadiliko katika mtindo wa maisha baada ya kuona dalili kwa kufanya mazoezi na mazoezi ni tiba ya vitu vingi iwe mara kwa mara dakika 30 kwa siku yanayofanya mwili kutoa jasho hayao yatasababisha damu kutembea mwili mzima na kupunguza mafuta mabaya mwilini,” amesema.

Amesema wanatakiwa kula vyakula bora vya matunda ya asili kulingana na misimu yake na kula mbogamboga hasa wanazozalisha nyumbani.

Aidha amewashauri kula vyakula vya jamii ya mbegumbegu kwani vingi ni vizuri mfano maharage ,soya na vitu vingine vyote ambavyo ni mbegu ni chanzo kizuri kuweka vizuri homoni za oestrojen.

“Tupendelee sana vyakula vya kujenga mwili vya protini kuna samaki ,maziwa na vingine baada ya mazoezi na kurekebisha mfumo wa chakula tujitahidi kupumzika kwa kulala masaa sita mpaka nane inasaidia kwa afya na kupunguza msongo wa mawazo.

“Vile vile kufanya kazi mbalimbali za jamii tukiacha kama biashara,kazi za ofisini tushiriki shughuli za kijamii kama kwenda kanisani ,kwenda kujadili mtaani,kulima bustani na zingine,”ameeleza.

Dk Lilian amesema ni vyema kula kwa kiasi kidogo vyakula vya wanga na mafuta.

“Nyama choma hizi mtu anaagiza kilo nzima au nusu kilo wale kwa kiasi wengine wanakula vyakula vya wanga kwa kiasi kikubwa pia wapunguze hasa wali ,”amesisitiza.

Amesema dalili nyingine za ukomo wa hedhi zinafatana na magonjwa mblimbali hivyo anasisitiza mwanamke anapoona dalili hizo afike kituo cha afya kuonana na mtaalamu na kufanyiwa uchunguzi, ushauri na tiba sahihi.

“Endapo itajulikana hana changamoto za afya isipokuwa ni mabadiliko ya kukoma hedhi basi tunambinu za kumsaidia kulingana na shida aliyopata huyo mwanamke .Kwanza kabisa nasisitiza wafike kituo cha afya kwa mfano kuna dalili za kutoka damu bila mpangilio inaweza kuashirika shida nyingine kubwa mfano saratani ya mlango wa uzaz,”amebainisha Dk Lilian.

Amesema mtaalamu wa afya ndio mwenye uwezo wa kukuambia una tatizo gani baada ya uchunguzi.

Dk Lilian amesema ni muhimu kuzingatia ushauri wa watalaamu na wenza waelewe kuna kipindi wanawake hawa wanapitia changamoto za kimaisha sio kwa kupenda ni kwasababu ya umri na maumbile au matibabu anayopitia.

“Unapoona mwenza wako amebadilika kihisia au kitabia ni vizuri kwenda naye taratibu na kujua changamoto zake ni nini na kuweza kukaa naye sawa,”amesema.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button