Maombi ya Mavokali yagusa mashabiki

DAR ES SALAAM : MSANII wa Bongo Fleva, Benjamin Mwenda maarufu kama Mavokali, ameacha gumzo mitandaoni baada ya kushiriki maombi ya dhati kupitia ukurasa wake wa Instagram, akimuomba Mungu msamaha na mwisho mwema wa maisha yake.

Katika chapisho hilo lililotolewa leo na kugusa hisia za mashabiki wengi, Mavokali alionesha unyenyekevu mkubwa mbele ya Mungu, akieleza wazi kutoridhishwa kwake na dhambi alizotenda na kuomba rehema. SOMA: Uwoya: Mafanikio ni maombi, matendo

Amesema hana uwezo wa kutimiza maagizo yote ya Mungu kikamilifu, hivyo anaomba Mwenyezi Mungu amchukue wakati atakapomridhia, ikiwa ni ishara ya kukubali udhaifu wa kibinadamu na kutegemea nguvu ya Mungu pekee. Miongoni mwa maombi yake yaliyogusa wengi, msanii huyo alitaja msamaha kwa dhambi zake zote ambazo za siri na zile za wazi na kumuomba Mungu aendelee kumfunika na kumlinda katika maisha yake ya kila siku.

Katika sehemu nyingine ya ombi hilo, Mavokali aliomba apate mauti yenye wepesi na asiwe na maumivu makali wakati wa kuaga dunia, hatua iliyoonesha imani yake ya kina na maandalizi ya kiroho. Maombi hayo yametafsiriwa na mashabiki wake kama ujumbe mzito unaohimiza tafakari ya maisha, unyenyekevu mbele za Mungu na umuhimu wa kutubu kabla ya mwisho wa safari ya dunia.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button