Mazungumzo mabadiliko matumizi ya mafuta kwenda gesi

SERIKALI kupitia Wizara ya Nishati imesema imekuwa na mazungumzo na Wizara ya Fedha kupunguza gharama na kodi katika vifaa vinavyotumika kubadilisha mfumo wa vyombo vya usafiri wa moto kutoka kutumia mafuta hadi gesi.

Naibu Waziri wa Nishati wa Nishati Salome Makamba amesema hayo wakati alipotembelea kituo mama cha kujaza gesi kilichopo eneo la Mlimani City jijini Dar es salaam.

Amesema kuna mpango ifikapo Jun, 2026 Mkoa wa Dar es salaam kila barabara kubwa iwe na vituo vya kujaza gesi ambapo pia kuna mpango wa kujenga vituo vikubwa Morogoro, Dodoma, Moshi, Tanga na Arusha.

Aidha Makamba amesema sekta binafsi zijitokeze kuwekeza kwenye eneo hilo kwani lina tija kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla hivyo wasisite kuwekeza kwani kwa sasa vijana wengi wamechangamkia fursa hiyo ya kutumia gesi hiyo kwenye vyombo vya moto.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) mpango wa Shirika ni kusambaza huduma hiyo ya gesi takriban barabara zote kubwa zinazoingia na kutoka jiji la Dar es salaam matarajio ni sekta binafsi kuweka vituo kwenye mikoa ya jirani.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button