Mazungumzo mapya Gaza wiki ijayo

CAIRO : SHIRIKA la habari la Al-Qahera, lenye uhusiano na serikali ya Misri, limeripoti kuwa mazungumzo ya amani ya Gaza yanatarajiwa kuanza tena wiki ijayo baada ya Israel kupitia majibu ya wanamgambo wa Hamas.

Kwa mujibu wa shirika hilo, ujumbe wa Israel umeondoka Misri siku moja baada ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kuwaita nyumbani wajumbe wake kwa mashauriano zaidi. SOMA: UN yaridhia Israel kuondoka Palestina

Mshirika mkuu wa Israel ambye ni Marekani imewarudisha wajumbe wake kwa mashauriano, huku mjumbe wa Marekani kwa Mashariki ya Kati Trump Steve Witkoff akiishutumu Hamas kwa kushindwa kuchukua hatua zinazofanikisha mazungumzo hayo.

Hata hivyo, Hamas imesema imeshangazwa na kauli hiyo, ikisisitiza kuwa msimamo wake umekaribishwa na wapatanishi na umefungua milango ya makubaliano.

Pande zote mbili, Israel na Hamas, zinakabiliwa na shinikizo kubwa la ndani na nje kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano yanayokaribia kuingia mwaka wa pili.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button