Mbaroni akidaiwa kuua rafiki, kuiba Sh Mil 61

DAR ES SALAAM: POLISI Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, imemkamata na kumuhoji Mussa Khamis Bakari, mkazi wa Temeke akituhumiwa kumuua rafiki yake Abdallah Twahir Selemani na kuiba Sh Milioni 61 zilizokuwa kwenye akaunti yake.

Kamanda wa Polisi kanda hiyo, SACP Jumanne Muliro akizungumzia historia ya tukio hilo, amesema Mei 1, 2024, majira ya saa 10:20 asubuhi, maeneo Mbutu Kichangani, Kigamboni, pembezoni mwa barabara itwayo Cheka kuelekea fukwe ya Kichangani uliokotwa mwili ambao baadaye ulitambuliwa ni wa Abdallah Twahir Selemani mkazi wa Chanika.

Soma: Auawa kwenye baa yake kwa wivu wa mapenzi

“Jeshi la Polisi lilipokea taarifa ya kupotea kwa Abulllah Twahir Selemani kutoka kwa mama yake, kuwa alipotea katika mazingira ya kutatanisha. Uchunguzi wa Jeshi la Polisi baadae uligundua kuwa tarehe 30 Aprili 2024, mtuhumiwa Mussa Khamis Bakari alikuwa na marehemu wakitumia gari namba T.928 DFY Suzuki Kei, wakitokea Magomeni kuelekea Temeke, Kijichi mpaka eneo ulipokutwa mwili wa marehemu”.

“Uchunguzi wa vitu mbalimbali umebainisha mtuhumiwa alimuua na baadae kwenda kutupa mwili huo pembezoni mwa barabara ulipookotwa,” amesema Kamanda Muliro.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by HABARILEO (@habarileo_tz)

“Baada ya kumuua, mtuhumiwa alichukua kadi ya benki ya marehemu na kwa nyakati tofauti tofauti alianza kutoa pesa kiasi cha shilingi Milioni 61 kutoka kwenye akaunti ya marehemu. Chanzo cha mauaji ni tamaa ya kutaka kuiba pesa kutoka kwa rafiki yake ambaye sasa ni marehemu,” amesisitiza kamanda Muliro.

 

Habari Zifananazo

Back to top button