Mbatia avuliwa uanachama NCCR Mageuzi

MKUTANO Mkuu wa Chama cha NCCR Mageuzi, umemvua uongozi na kumtimua uanachama, aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, James Mbatia, wakati Makamu wake Angelina Rutairwa akivuliwa wadhifa wake.

Pia mkutano huo ulitaka viongozi wote waliohusika na ubadhirifu wa mali akiwemo Mbatia kuchukuliwa hatua za kisheria.

mkutano huo Umempitisha kwa kauli moja mwanachama  Haji Ambari Hamisi, kuwa Mwenyekiti wa chama hicho huku Joseph Selasini akichaguliwa kuwa Makamu wake kwa kura 173.

Mkutano huo unafanyika leo Jumamosi Septemba 24, 2022 jijini Dodoma na kuhudhuriwa na wajumbe 224 kati ya 368 waliopo kwa mujibu wa Katiba ya chama chao.

Wajumbe walifanya hivyo baada ya Kaimu Mwenyekiti wa chama hicho Haji Ambari Hassan kutaja tuhuma saba zinazomkabili Mbatia na tuhuma mbili za Angelina.

Miongoni mwa mashtaka yanayomkabili Mbatia ni kuuza mali za chama, ikiwemo mashamba na nyumba katika maeneo mbalimbali.

Ambari amewaambia wajumbe hao kuwa viongozi hao walipelekewa hati ya mashtaka yao na walitakiwa kujibu ndani ya siku 14 kama katiba yao inavyotaka.

Hata hivyo, amesema kuwa hakujibu mshtaka hayo na wala hakufika katika mkutano huo,  licha ya kualikwa, ili aweze kujitetea mbele ya wajumbe.

“Tumewaita katika mkutano huu, lakini hawakutaka kuja na badala yake walikimbilia mahakamani kuzuia kwa mara nyingine mkutano huo,” amesema.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x