Teknolojia ya IVF yaokoa kizazi

LONDON : WATOTO wanane wenye afya nzuri wamezaliwa nchini Uingereza kupitia mbinu mpya ya upandikizaji wa mimba (IVF), ambayo imefanikiwa kupunguza hatari ya watoto kurithi magonjwa ya vinasaba kutoka kwa mama zao.
Mbinu hiyo ya kisasa imeelezwa kuwa mafanikio makubwa katika nyanja ya tiba ya uzazi na vinasaba, na inatoa matumaini kwa wanawake wanaobeba magonjwa ya kurithi kupata watoto bila kuwaambukiza watoto wao maradhi hayo.
Kwa mujibu wa watafiti walioko Uingereza, teknolojia hiyo imeweza kuzuia uhamishaji wa magonjwa yanayosababishwa na hitilafu katika DNA ya mitokondria aina ya vinasaba vinavyopatikana katika seli na hurithiwa kutoka kwa mama.
SOMA: Serikali yajizatiti kupunguza vifo vya uzazi
Wataalamu wamesema mafanikio hayo yanatoa dira mpya kwa familia nyingi duniani, ambazo zimekuwa zikiathiriwa na magonjwa sugu ya kurithi ambayo mara nyingi hayana tiba ya moja kwa moja.



