Mbio nishati safi zaiva Arusha

ARUSHA: MKUU wa Mkoa wa Arusha, Kenani Kihongosi amewaaalika wananchi mbalimbali kujitokeza kushiriki mbio za riadha za Nishati Safi ya Kupikia zilizopangwa kufanyika Agosti 3 Njiro.

Akizungumza jana, RC Kihongosi alisema katika kuelekea Sikukuu ya Nanenane kutakuwa na  mbio ambazo zitahusisha km 21, km 10 na km 5.

“Pia kuanzia Agosti 2 hadi 8 kutakuwa na mabanda  ya teknolojia ya nishati safi ambayo yatafanyika  eneo la  Nanenane Njiro na kuwahisi wananchi wote wa mikoa  ya jirani  ikiwemo Manyara na Kilimanjaro  na Arusha yenyewe  kuja kushiriki.

Alieleza kuwa pia kutakuwa na mafunzo ya matumizi ya nishati safi na elimu itatolewa kuhusiana na  madhara ya kutumia nishati isiyosafi

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Business Women Association (TABWA) ambao ndio waandaaji, Noreen Mawalla amesema mbio hizo za kihistoria ni kuhamasisisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa maendeleo ya mwanamke na Taifa kwa ujumla ambapo ni msimu kwanza  toleo la pili na  tayari  zimefanyika jijini Dar es salaam , ambapo watu 436 walishiriki.

“Tukio hili linafanyika kama sehemu ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Nishati Safi ya Kupikia, inayolenga kuhakikisha kuwa zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ifikapo mwaka 2032.

Aidha, juhudi hizi ni mwitikio wa wito wa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye ni kinara wa mapambano ya kuondoa matumizi ya kuni na mkaa barani Afrika, kupitia kaulimbiu yake maarufu: “Tumtue Mama Kuni Kichwani.” amesema Mawalla.

Alisema Clean Cooking Marathon ni sehemu ya kampeni ya kitaifa inayotarajiwa kufanyika katika kanda zote 5 za Tanzania, ikilenga  kuelimisha jamii juu ya athari za matumizi ya nishati chafu, kuongeza ufahamu kuhusu nishati mbadala, na kushirikisha wadau mbalimbali katika kuharakisha na kuchochea mabadiliko chanya.

“Kauli mbiu ni Nishati safi ya kupikia,Linda Afya ,hifadhi mazingira kwa uchumi endelevu  na tunatoa  wito kwa wananchi wote, mashirika, na sekta binafsi kushiriki kwa wingi kuelekea kilele cha mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Agasti 3 mwaka huu eneo la  Njiro, Arusha,”ameongeza Mawalla.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button