Mbio za Meru Pazuri kusaidia watoto njiti

ARUSHA: MBIO za Meru Pazuri maalumu kwa ajili ya kusaidia watoto wanaozaliwa njiti zitafanyika Septemba 21, 2025 wilayani Arumeru mkoani Arusha.

Zikijulikana kama ‘Meru Pazuri Afya Marathon and Festival ‘ zitahusisha kilometa 21,kilimeta 10 na kilometa 5 zimeandaliwa na wadau wa maendeleo katika Halmashauri ya Meru ambapo mbali na kulenga kuchangia vifaa kwa watoto wanaozaliwa njiti pia zitahusisha burudani mbalimbali .

Zaidi ya wakimbiaji 500 na washiriki 2000 wa matukio ya burudani mbalimbali kutoka ndani na nje ya Arusha wanatarajiwa kushiriki tukio hilo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Mbio hizo, Goodluck Sommy amesema mbio zitafanyika uwanja wa Shule ya Msingi Kilimani, Leganga Halmashauri ya Wilaya Meru na kusema maandalizi yanaenda vizuri kwani tayari wamewasiliana na Mganga Mkuu wa Wilaya pamoja na mratibu wa afya ili kuona jambo linafanyika vyema.

“Lengo kuu ni kuwachangia vifaa watoto wanaozaliwa njiti vifaa katika hospitali yetu ya Wilaya ya Arumeru kwa ajili ya kuwasaidia na tunaamini vifaa hivi vitakuwa msaada mkubwa na si Meru pekee hapa tu bali Mkoa wa Arusha na hata nchi nzima kwa ujumla,”amesema Sommy.

Amesema ni mbio ya kwanza na itakuwa endelevu hivyo waliona wafanye kipaumbele kuwachangia watoto hao ambapo aliwaomba wadau wote wa afya waungane nao pamoja kwa ajili ya kufanikisha jambo hilo.

Aidha, alisema mbio hizo pia ni katika kuimarisha afya.

Naye Mjumbe mhamasishaji wa Meru Pazuri Afya Marathon and Festival Amos Daniel ameleza kuwa Meru kuna vivutio vingi ikiwemo hifadhi ya Taifa ya Arusha National park, Ziwa duluti ,msitu wa Asili hivyo ni vitu vitaweza kuwahamasisha kwa wanaotoka maeneo mbalimbali kuja kufurahia na kuburudika.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button