Dk Samizi awatembelea majeruhi ajali ya basi, lori Moro

NAIBU Waziri wa Afya, Dk Florence Samizi, kwa niaba ya Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa, ametembelea na kuwajulia hali majeruhi wa ajali ya basi na lori iliyotokea usiku wa Desemba 31, 2025 katika kijiji cha Maseyu, mkoani Morogoro.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Dk Samizi amesema hadi Januari 2, majeruhi 5 wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, majeruhi 2 wamepewa rufaa kwenda Taasisi ya mifupa Muhimbili kwa matibabu zaidi, huku majeruhi 16 wakiruhusiwa kurejea majumbani baada ya hali zao kuimarika.

Aidha, Kuhusu marehemu, amesema kuwa miili 4 tayari imetambuliwa, ambapo miili 3 imekabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya mazishi.

Ameongeza kuwa miili 6 ilichukuliwa vinasaba (DNA) kwa ajili ya utambuzi, na kati ya hiyo mwili 1 tayari umetambuliwa, huku ndugu wakisubiri kukamilika kwa taratibu za Kipolisi ili kuuchukua. Kwa sasa, miili 5 inaendelea kusubiri majibu ya vinasaba.

Naibu Waziri ametoa wito kwa ndugu na jamaa wa marehemu ambao bado hawajatambulika kufika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kusaidia zoezi la utambuzi wa miili na kukamilisha taratibu za mazishi.

Katika ziara hiyo, Dk Samizi amesema majeruhi waliopata fursa ya kuzungumza naye wamemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kuboresha sekta ya afya hali iliyopelekea wao kupata huduma bora, za haraka na kwa wakati mara baada ya ajali kutokea.

Aidha, amewapongeza na kuwashukuru watendaji wa sekta ya afya kwa kujitoa kwao katika kuwahudumia majeruhi kwa wakati, huku akiwataka madereva kuendelea kuzingatia sheria za usalama barabarani na kuchukua tahadhari wanapotumia barabara.

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. l Get paid over $110 per hour working from home. l never thought I’d be able to do it but my buddy makes over $21269 a month doing this and she convinced me to try. The possibility with this is endless….

    This is what I do………………………………….. ­­­https://Www.Cash54.Com

    1. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
      .
      M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com

  2. l Get paid over $110 per hour working from home. l never thought I’d be able to do it but my buddy makes over $21269 a month doing this and she convinced me to try. The possibility with this is endless….

    This is what I do………………………………….. https://Www.Cash54.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button