Mbogwe walia na mitandao ya simu

GEITA: UONGOZI wa Halmashauri ya Mbogwe imelia na changamoto ya mitandao ya simu ambayo inasababisha kudhohofu kwa utendaji wao.

Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Sakina Mohamed akielezea changamoto za wilaya hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela ambaye yupo wilayani humo kwa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo amesema kutokuwepo kwa mitandao ya simu katika makao makuu hayo kunasababisha gharama kubwa kwa wananchi kufuata huduma katika Makao Makuu ya Halmashauri kwani wananchi walio wengi wako eneo la Masumbwe ambapo ni zaidi ya KM 40 kutoka yalipo makao makuu.

Aidha, amesema pia changamoto nyingine iliyopo katika wilaya hiyo ni ubovu wa miundombinu ya barabara inayoenda katika makao makuu ya wilaya hiyo.

Katika kuifanyia kazi changamoto hiyo, Shigela amewalekeza TTCL kuhakikisha wanaharakisha ujenzi wa minara kwenye makao makuu hayo ya Halmashauri lakini pia kuwataka TANROAD kuweka mipango thabiti ili kuharakisha ujenzi wa barabara ili wananchi wasi_gharamike.

Katika hatua nyingine, Shigela amekagua miradi mitatu ikiwemo nyumba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo ambayo imegharimu Sh milioni 150, nyumba za wakuu wa idara sita pamoja na hospitali ya Wilaya ya Mbogwe ambayo ujenzi wake uko katika hatua za mwisho huku ikigharimu zaidi ya Sh bilioni 2 pamoja ujenzi wa mradi wa Shule ya msingi Majengo unaojengwa kupitia mpango wa BOOST wenye thamani ya Sh milioni 540.
……

Habari Zifananazo

5 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button