Mbunge alia na kero ya popo Dar

MBUNGE wa Viti Maalum,William Mgaya amehoji bungeni ni lini serikali itaondoa popo waliopo maeneo ya Upanga, Dar es Salaam ili kulinda afya za wakazi wa eneo hilo.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Danstan Kitandula, amesma wizara imeendelea kudhibiti popo katika Jiji la Dar es Salaam kwa kuchukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufanya soroveya ya kuangalia ukubwa wa tatizo, maeneo yaliyoathirika, mbinu gani ambazo ni rafiki kwa mazingira zitumike kudhibiti na pia kubaini aina ya popo wanaosumbua.

‘’Imebainika kuwa kuna aina mbili (2) ya popo wanaosumbua, ambao ni popo wanaokula matunda (hawa wanaotumia miti kama maeneo yao ya makazi) na popo wanaotumia mapango au magofu ya nyumba kama makazi yao.

‘’Katika kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo, majaribio ya dawa tano (repellents) za kunyunyizia ili kufukuza popo katika makazi yao (roosting sites) zilitumika.

‘’Kati ya dawa hizo; dawa mbili (Napthalene na Bat CRP) zimeonekana kuwa na uwezo wa kuwafukuza popo hao na juhudi zaidi zinaendelea kwa kushirikiana na wadau kwenye maeneo husika,” amesema.

Habari Zifananazo

4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button