Mbunge alia na utapeli wa ardhi Bagamoyo

DODOMA; MBUNGE wa Jimbo la Bagamoyo, Muharami Mkenge, amesema wananchi wengi wanauziwa maeneo ya ardhi Bagamoyo mkoani Pwani kwa kutapeliwa na baadaye ndiyo wanaoumia.

Amesema katika jimbo lake maeneo makubwa yenye migogoro ya ardhi ni Mapinga na Makurunge, ambapo kuna uvamizi mkubwa wa mashamba na kisha wananchi kuanzisha ujenzi, ambapo baada ya muda masuala hayo yanakwenda katika mahakama na kutolewa uamuzi wa kuvunjwa nyumba.

Akichangia bungeni hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi mwaka 2023/24, leo bungeni mjini Dodoma, amesema wananchi wanyonge ndiyo wanaoumia kwa kuuziwa maeneo na baadaye kuvunjiwa.

Isome pia: https://habarileo.co.tz/waziri-silaa-aja-na-vipaumbele-5-ardhi/

Amesema wanatumia miaka mingi kufanya ujenzi, lakini nyumba zinavunjwa kwa dakika tano tu, hivyo kumuomba Waziri Silaa kasi yake katika wizara hiyo pia aangalie masuala ya utapeli wa ardhi unaofanywa na waabdhi ya watu.

Mbunge huyo amesema kuna eneo Mapinga ambalo umiliki wake wa ardhi umebadilishwa na limerudishwa serikalini na kusema ni vyema sasa wananchi ambao wamejenga katika eneo hilo warasimishwe maeneo yao, kwani kuna nyumba zaidi ya 4,000 zimejengwa.

 

Habari Zifananazo

Back to top button