SERIKALI imeshauriwa kuangalia uwezekano wa kuongeza kampuni nyingine ya mabasi yaendayo haraka ili kupunguza changamoto ya upatikanaji wa huduma hiyo kwa wakazi wa Dar es Salaam.
Ushauri huo umetolewa leo Oktoba 29, na Mbunge wa Jimbo la Iramba Mashariki mkoani Singida, Francis Mtinga wakati akizungumza bungeni jijini Dodoma.
“Mtu unaenda kwenye kituo unakaa muda mrefu, na hii kwa sababu labda ni kampuni moja, hebu tuiombe serikali ziwepo kampuni kadhaa zianze kushindana,” amesema Mtinga.
Mtinga amesema suala hilo linapaswa kuchukuliwa kwa uzito kutokana na miundombinu ya kisasa na fedha ambazo serikali inawekeza kwenye miradi hiyo.