Mbunge awavuta wafanyabishara sekta ya madini

MBUNGE wa Jimbo la Ulanga mkoani Morogoro, Salimu Hasham amewavuta wafanyabiashara  kuwekeza katika sekta ya madini ya Spinel yanayochimbwa katika kijiji cha Ipango Mahenge kwani yana thamani kubwa kuliko madini ya Tanzanite.

Hasham ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Kuuza, Kununuwa na kuchimba madini nchi ya Ruby International LTD amesema ni wakati wa wafanyabiashara kutoka nje na ndani kujitanuwa ikiwa ni pamoja na kujikita katika aina hiyo ya madini.

Hasham amesema uchimbaji wa madini aina ya spinel haukuanza hivi karibuni bali ameianza Yeye akiwa mdogo sana wakati huo maeneo hayo ambayo hivi sasa wanachimba huko nyuma walikuwa wanatembea Kwa miguu kuelekea kwenye makazi ya watu.

“Madini Spinel haijaanza leo ni vile tu watu walikuwa hawajuwi kwamba Kuna madini yanaitwa spinel hivi sasa yameingia sokoni na yanaonekana kama mahitaji yake ni makubwa na uchimbaji wake ni mgumu kidogo na hata upatikanaji wake sio rahisi na gharama za uendeshaji ni kubwa pia na madini hayo yanagharama kubwa zaidi kuliko madini ya Tanzanite “,amesema

Akizungumzia safari yake nchini Thailand kwa ajili ya soko la madini hayo ya vito Mbunge Hasham alisema madini ya spinel hitaji lake ni kubwa duniani na soko lake pia na madini hayo yanachimbwa kwenye nchi tatu ambazo ni pamoja na Tanzanaia ,Bama, na vetinam.

Akitolea mfano upande wa gharama za uendeshaji katika uchimbaji na kusema kuwa mwaka jana walikuwa wananunua Sh 2,300 kwa lita ila leo mafuta yanakwenda mpaka Sh 3500 hivyo hatuwezi kila siku unauza madini ya gram moja kwa Sh milioni 1 wakati mafuta yamepanda manaake hawawezi kuendelea kufanya kazi hiyo hivyo lazima wapandishe thamani ya madini hayo.

Amesema yey kama mbunhe ataendelea kuikumbusha serikali kufanyia kazi changamoto katika Sekta ya Madini hususani suala la umeme wa uhakika mgodini Ipango kwani kukosekana kwa nishati hiyo kunaongeza gharama za uendeshaji.

Akimzungumzia Rais Samia kuhusu mwelekeo wa nchi kupitia sekta ya madini 2030 amempongeza Rais kwani Royal Tour imeweza kutangaza sekta hiyo Kwa kiasi chake.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
MaryRyder
MaryRyder
26 days ago

I’ve gained only within four weeks by comfortably working part-time from home. Immediately when I had lost my last business, mtg I was very troubled and thankfully
following website___________ http://Www.Careers12.com

Last edited 26 days ago by MaryRyder
Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x