Mbuyu, mti wenye hadithi nyingi za kipekee

Mbuyu ni mti uliojaaliwa sifa za kipekee katika miti yote duniani kutokana na kuwa na matumizi mengi sambamba na kuwa moja ya miti inayoishi muda mrefu zaidi unaokadiriwa kuzidi miaka 2,000.
Ninaweza kusema kwamba mti huo umekuwa na faida nyingi katika maisha ya binadamu hasa kwa nchi za Afrika.
Faida za mti huo ni pamoja na kutumika kwa chakula. Katika maeneo mbalimbali ya Tanzania hasa vijijini, majani ya mbuyu yamekuwa yakitumika kama mboga na magome yake yakitumika kutengeneza dawa za asili kwa ajili ya kutibu magonjwa mbalimbali.
Matumizi ya kiutamaduni
Mtandao wa TRT Afrika unabainisha kuwa katika maeneo mengi nchini Nigeria majani ya mbuyu yamekuwa yakitumika kama mboga au unga wake kama kiungo cha supu na mbegu zake zimekuwa zikitumika kwa uji au juisi.
Pia, inaelezwa magome ya mbuyu yanaweza kutumika kutengeneza nyuzi kwa ajili ya kutengeneza kamba za kufuma vikapu na kuezeka paa za nyumba.
Hata hivyo, inaaminiwa nchini humo kuwa wakati mwingine mbuyu una sifa mbaya kitamaduni ukihusishwa na ushirikina, ikiwa ni pamoja na kuhusishwa na roho za wafu, imani za mizimu na majini.
Hisia hizo si kwa Nigeria peke yake, bali hata Tanzania ambako mbuyu umekuwa ukihusishwa na makazi ya majini hasa kwa ile iliyozeeka na kuwa na mashimo kwenye mashina yake, mashimo yakielezwa kuwa ndiyo makazi ya majini.
Pia, inaaminika miongoni mwa baadhi ya jamii za Watanzania kuwa mibuyu ni makutano ya wachawi wanapokuwa na mikutano yao usiku.
Hadija Nguzo mwenye umri wa miaka 82 anasema katika maisha yake yote tangu akiwa binti mdogo wamekuwa wakiaminishwa kwamba mibuyu siyo miti mizuri kwani ni makazi ya majini na wachawi wamekuwa wakiitumia kufanya shughuli zao za kichawi.
“Tulikatazwa kupita au kucheza kwenye mibuyu mchana, hasa ikifika saa sita mpaka saba, jua likiwa kali sana. Mzazi akikukuta utaadhibiwa vibaya mno,” anasema.
“Na tulikuwa tunaamini kabisa! Kama unapita njia ina mbuyu majira ya mchana unakuwa makini sana saa sita, saba isikukute kwenye mbuyu na wakati mwingine wale waliokuwa wanaishi karibu na mibuyu walikuwa wakisikia harufu za vyakula vya mitaani huko mchana wa jua kali, wanaamini inatoka kwenye mbuyu na majini ndiyo wanapika,” anasema huku akiachia kicheko kikali.
Kwa upande wangu nathubutu kusema mti huo ni wa kipekee kutokana na namna ambavyo nimekuwa nikiishi na kushuhudia mambo yanayotendeka katika miti hiyo.
Miti hiyo ambayo ina tabia ya kutengeneza mashimo kwenye shina pindi inapozeeka nimekuwa nikiona ikitumika kwa mambo mbalimbali ya utamaduni, ikiwemo jando kwa makabila mbalimbali yanayoishi maeneo yenye miti hiyo.
Mwaka 1994 nikiwa kijijini kwa bibi yangu Kingiti, Mpwapwa mkoani Dodoma nilishuhudia sherehe za jando ambako ngoma zilipigwa na kuchezwa pembeni ya mbuyu mkubwa ambao ni maarufu kwa shughuli hizo kijijini hapo.
Mbuyu huo una shimo kubwa lenye uwezo wa kuingiza takribani watu wanne hadi sita. Hii ni kutokana na ukubwa wa shina la mti huo.
Hiyo ni kawaida kwani shina la mbuyu uliokomaa linaweza kufikia ukubwa wa kuzungukwa kwa kukumbatiwa na watu hata 20 waliotanua mikono yote miwili kwa kuinyoosha kulia na kushoto. Sababu ya kutokea kwa shimo hilo kwa mujibu wa watafiti ni kushambuliwa na magonjwa lakini kutokea kwa shimo hilo kunakuwa na faida kwa baadhi ya watu wanaotumia mibuyu kwa shughuli za jando na matambiko.
Mti wa mbuyu unaweza kupewa sifa ya ‘mti wa uzima’ kumaanisha mti unaoishi muda mrefu sana ukihimili hali zote za hewa hususani katika maeneo ya Savana.
Mti huo umepewa uwezo wa kuhimili kiangazi kikali na kuufanya upukutishe majani bila kufa, hiyo ni kwa sababu mbuyu una uwezo wa kujihifadhia maji na chakula katika shina kwa kipindi hicho, hali inayoufanya uweze kuhimili hadi wakati wa mvua ambapo huchipua majani machanga na kuzalisha maua na matunda tena.
Unapoukuta mbuyu wakati wa kiangazi unaweza kusema hautaweza kutoa majani mengine tena na pengine utakufa moja kwa moja lakini ni kinyume chake, mbuyu umepewa uwezo kuibua uhai wake kutoka wakati wa kiangazi hadi masika.
Inaelezwa kuwa mbuyu mmoja unaweza kuishi hata zaidi ya miaka 3,000 na unaweza kujua umri wa mbuyu kwa kutumia mikono ya mwanadamu.
Ofisa Uhifadhi katika Hifadhi ya Kisiwa cha Lundo kilichopo Mbambabay, Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma, Maajabu Mbogo anasema ili kujua umri wa mbuyu mtu anapaswa kukumbatia mbuyu kwa mikoni yote na kila kumbato moja linahesabiwa ni sawa na umri wa miaka 100.
“Ukitaka kujua umri wa mbuyu wowote ule unatanua mikono yako yote miwili halafu unaenda kuukumbatia ule mti, mikono yako itakapoishia basi hicho ni kiashiria cha miaka 100 ya uhai wa huo mbuyu,” anasema.
Akitolea mfano kwa mmoja wa mibuyu iliyoko katika ufukwe wa Ziwa Nyasa katika Kijiji cha Lipingo, Maajabu alikusanya watu 17 na kukumbatia mbuyu huo kwa kuuzunguka, hiyo ikimaanisha mbuyu huo umeishi kwa miaka 1,700 lakini ukionekana kama hauna miaka mingi.
Hiyo ni uthibitisho kwamba mbuyu ni mti unaoishi miaka mingi sana bila kufa na ili kuua mbuyu itakulazimu uukate na kuhakikisha umeng’oa mizizi yake na kuiharibu kabisa, kinyume na hapo mbuyu ukikatwa mvua ikinyesha unatoa majani na matawi mapya na kuendelea kuishi.
Hatari ya kutoweka
Pamoja na ustahamilivu katika kuishi kwake, mti huo umekuwa katika hatari ya kutoweka hasa kutokana na maenedeleo ya miji na mahitaji zaidi ya ardhi na kufanya idadi kubwa ya miti hiyo ipungue.
I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
This is what I do———⊃⫸ http://Www.EarnApp1.Com
Earn extra cash every week from the comfort of your home! This flexible part-time opportunity is perfect for anyone looking to make 300-1300 Dollars weekly. Start now and receive your first payment in just a few days. Don’t miss out—join today. Tap on Finance Economy OR Investing.
Here’s what I do……………….. http://Www.CartBlinks.com
JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… Y You can earn from 6000-12000 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good eaning opportunity.tab for more detail thank you……..
For details check ——-⫸ http://www.get.money63.com
I’m making $23000 to $29000 a month working part time. I kept hearing other people tell me how much money they ws can make online so I decided to look into it. Well, it was all true and has totally changed my life. First month i received $24758 just working on the laptop for 3 hours per day.
This is what I do…………..www.get.money63.com
I’m making $23000 to $29000 a month working part time. I kept hearing other people tell me how much money they ws can make online so I decided to look into it. Well, it was all true and has totally changed my life. First month i received $24758 just working on the laptop for 3 hours per day.
This is what I do…………www.get.money63.com
Wonderful web site. Lots of helpful information here. I’m sending it to some pals ans additionally sharing in delicious. And certainly, thank you to your sweat!