Salim Asas apiga kura, apongeza uchaguzi amani

IRINGA: Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Salim Asas, leo amepiga kura katika kituo cha Chuo cha Afya kilichopo kata ya Gangilonga, Manispaa ya Iringa, na kuipongeza jamii ya Iringa na Watanzania kwa ujumla kwa namna wanavyoshiriki uchaguzi huo wa amani, utulivu na heshima.

Akizungumza mara baada ya kupiga kura, Asas alisema kuwa hali ya uchaguzi ni shwari kabisa, na kwamba anaiona Tanzania ikiendelea kuwa mfano wa kuigwa katika siasa za kidemokrasia barani Afrika.

“Nimepiga kura yangu kwa utulivu mkubwa. Zoezi linaenda vizuri sana, hakuna vurugu, hakuna maneno mabaya. Huu ni ushahidi kwamba taifa letu limekomaa kisiasa na Watanzania wanathamini amani kuliko kitu chochote,” alisema Asas.

Aliongeza kuwa kwa mara ya kwanza katika historia ya chaguzi nchini, kumekuwa na utulivu wa hali ya juu, huku akiwataka wananchi wote kuendelea kujitokeza kwa wingi kutekeleza haki yao ya kikatiba kwa amani na upendo.

“Tuna muda hadi jioni. Kila mtu ajitokeze kupiga kura bila woga, kwa sababu usalama upo wa kutosha. Tukimaliza tutarudi majumbani tukiwa tumetimiza wajibu wetu kwa nchi yetu,” alisisitiza.

Katika kituo cha Chuo cha Afya, wananchi wa rika mbalimbali walionekana wakifika kwa wakati, wakiwa na mstari wa nidhamu tangu asubuhi. Wengine waliopiga kura katika kituo hicho ni Balozi, Dk Pindi Chana, na viongozi wengine waandamizi wa CCM.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, alisema hali ya usalama katika mkoa huo ni tulivu na thabiti, akiwahakikishia wananchi kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vipo kazini kuhakikisha kila kitu kinaenda kwa amani.

“Zoezi linakwenda vizuri, watu waendelee kujitokeza kupiga kura kwa utulivu. Kura zitahesabiwa kwa usalama na matokeo yatatangazwa kwa usalama. Niwasisitize tusibomoe amani tuliyoijenga kwa miaka mingi,” alisema RC James.

Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, Zaina Mlawa, aliwapongeza maafisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) akisema wanatekeleza majukumu yao kwa weledi mkubwa, na wananchi wameonyesha nidhamu ya hali ya juu katika vituo mbalimbali vya kupigia kura.

Zoezi hilo la Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, linahusisha kuwachagua viongozi katika ngazi mbalimbali za uongozi, wakiwemo Madiwani, Wabunge na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ulinzi uliimarishwa ipasavyo, huku askari wakihakikisha kila kitu kinaenda kwa utulivu na amani, jambo linalotoa taswira chanya kwa taifa zima kuwa Tanzania bado ni ngome ya amani, umoja na demokrasia ya kweli.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..

    .

    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us →→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button