Serikali ya mpito kuanza kujadiliwa

NEPAL : HALI ya utulivu imeanza kurejea nchini Nepal siku chache baada ya waandamanaji kuipindua serikali na kuchoma moto majengo ya umma, yakiwemo Bunge na ofisi za serikali. Kwa sasa, wawakilishi wa waandamanaji wanafanya mazungumzo na viongozi wa jeshi katika makao makuu ya jeshi mjini Kathmandu, kwa lengo la kupata kiongozi wa mpito.
Maandamano hayo yalichochewa na hatua ya serikali kutumia vyombo vya usalama kukandamiza maandamano ya vijana waliopinga marufuku ya mitandao ya kijamii, ambapo watu 19 waliuawa.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Wizara ya Afya nchini humo imesema idadi ya waliopoteza maisha mpaka sasa imefikia 25. Shinikizo hilo la wananchi limemfanya Waziri Mkuu Khadga Prasad Oli kujiuzulu na kukimbia. SOMA: Rubani apona ajali ya ndege Nepal



