Mchinjita ashinda makamu mwenyekiti Bara

MKUTANO Mkuu wa ACT Wazalendo umemchagua Isihaka Mchinjita kuwa Makamu Mwenyekiti Bara wa chama hicho kwa kupata kura 517 sawa na asilimia 96.1.
Nafasi ya Makamu Mwenyekiti Zanzibar imeenda kwa Ismail Jussa aliyeshinda kwa kura 509 sawa na asilimia 99.6 ya kura zote zilizopigwa.
Februari 16 mwaka huu, Mchinjita alichukuwa fomu kugombea nafasi hiyo ambapo moja ya ahadi zake zilikuwa ni kukijenga chama hicho ili kiendelee kuwa chama chenye kuibua masuluhisho ili wananchi wakiamini katika kuunda serikali.
Mchinjita ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ACT, awali kabla ya uchaguzi huo, alisema shauku yake ni kuimarisha sera na mwenendo wa chama hicho ili kibaki kuwa chama kinachosimama kama chama kiongozi kwenye kusukuma na kushinikiza utekelezaji wa agenda zenye maslahi kwa wananchi.



