‘Meno ni hazina yaking’oka kuna matamshi yatakushinda’

MTWARA; JE wajua kuwa ukiwa umepoteza meno au kung’oa kuna matamshi au maneno huwezi kutamka wakati unaongea?
Chama Cha Wataalamu wa Afya ya Kinywa na Meno Nchini (TDA) kimesema ikitokea mtu ameng’oa au kupoteza jino, mtu huyo anahitaji kuwekewa meno bandia ili kuweza kutamka maneno yote wakati anaongea.
“Ikitokea umepoteza jino basi unahitaji kuweka jino bandia, utakubaliana na mimi mtu ambaye anakosa meno kuna matamshi hawezi kutamka mathalani ukiwa huna meno ya mbele,” amesema Rais wa chama hicho Dk. Gema Belege.

Amesema licha ya kushindwa kutamka maneno, mtu ambaye amepoteza meno huathirika kiafya kwenye kinywa, meno na hata mwili mzima.
Dk. Gema amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya siku ya Afya ya Kinywa na Meno duniani inayoadhimishwa Machi 20 kila mwaka, ambapo kitaifa yatafanyika mkoani Mtwara.

Zaidi ya wananchi 100, mkoani Mtwara wamepatiwa huduma ya kuwekewa meno bandia bure na madktari bingwa wa TDA ili kurejesha afya ya kinywa na meno



