Mexime aula Ihefu

MBEYA: Kocha, Mecky Mexime amejiunga na Timu ya Ihefu kutoka Mbeya baada ya kuachana na Kagera Sugar siku kadhaa zilizopita.

Mexime anachukua nafasi ya, Moses Basena aliyesitishiwa mkataba  Desemba 05 mwaka huu.

Makocha watatu tayari wamepita Ihefu msimu huu ambapo walianza na Kocha,John Simkoko akatimka mwezi Septemba na kocha Zuberi Katwila akachukua usukani nae akaachana na wababe hao na kuibukia Mtibwa Sugar na nafasi yake ikachukuliwa na  moses Basena ambaye nae hajadumu ndani ya walima mchele hao wa Mbarali.

Mexime anakuwa kocha wanne kuiongoza Ihefu msimu huu.

 

Habari Zifananazo

Back to top button