Meya Mikindani aipongeza serikali maboresho afya, elimu

MEYA wa Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara, Shadida Ndile ameipongeza serikali kutokana na maboresho ya huduma mbalimbali kwa wananchi ikiwemo afya, elimu na mingine.
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka 63 ya uhuru wa Tanzania Bara yaliyofanyika kwenye manispaa hiyo ya mtwara Mtwara mikindani, meya huyo wa manispaa hiyo amesema kwa sasa serikali imekuwa na jitihada kubwa za kuboresha huduma hizo kwa wananchi ikilinganishwa na miaka ya nyuma.
Amesema serikali hiyo imejenga hospitali za rufaa ,vituo vya afya zahanati, nyumba za watumishi na kuongeza vifaa tiba lakini pia madarasa ya kutosha, barabara kwa viwango vya lami na mengine mengi hali inayopelekea wananchi kupata huduma bora zaidi kupitia huduma hizo.
Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mtwara Mjini, Fadhili Mrami amewasihi vijana wasomi kujitokeza kuwania nafasi za uongozi pale zinapotokea ili kupata nafasi za kusimamia shughuli za maendeleo ya taifa.
Emeliana Lenatus Mwanafunzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Mtwara, Emeliana Lenatus amethibisha uwepo wa mabadiliko katika sekta za afya ,elimu na kilimo kutokana na upatikanaji wa bima za afya, pembejeo kwa wakulima ambayo ni chachu ya maendeleo katika jamii.
“Tunaishukuru sana serikali yetu kwa kazi kubwa inayofanya kwasababu tunajionea maendeleo kupitia sekta mbalimbali kama vile ya afya na mingine mingi tu”amesema Lenatus
Maadhimisho hayo yameenda na kauli mbiu inayosema ‘Uongozi Madhubuti Ushilikishwaji wa Wananchi msingi wa maendeleo yetu”



