Mfahamu mwanahabari aliyepitia mikasa, vitisho

MIONGONI mwa changamoto wanazokutana nazo waandishi wa habari ni pamoja na mikasa ya kupigwa na vitisho kutoka kwa wadau na watu wanaofanya nao kazi.

Rajabu Robert Hezron ‘aka’ Rojamastory  ni miongoni mwa waandishi wa habari ambao anaelezea mkasa uliowahi kumkuta katika harakati zake za kikazi hatua iliyokatisha tamaa kipindi fulani lakini pia, alipata funzo kubwa kwenye maisha yake.

Akizungumza na Mwandishi wa HabariLeo Digital Roja amesema yeye ni mwandishi wa stori za burudani kutoka chombo cha mtandao wa Carrymastory na moja ya mkasa uliowahi kumkuta alifanya mahojiano.

Advertisement

Mahojiano hayo yalimhusisha mdau wa burudani na moja ya mastaa wakubwa nchini ambapo huyo mdau alikuwa anatoa maoni yake kumhusu msanii huyo jina tunalo, mapokeo yalikuwa tofauti na matarajio.

Kwa mfano ni kama wachambuzi wa soka wanavyowakosoa baadhi ya wachezaji halafu wachezaji husika wakasirike kupita kiasi na kuchukua hatua kwenda kwenye vyombo vya usalama ndivyo ilivyomkuta Roja.

Anasema kwa namna msanii alivyozungumziwa na mdau aliyehojiwa hakudhania kama angekasirika kwa kiasi kikubwa hadi kufikia hatua mashabiki wa msanii husika kutoa vitisho vya kutaka kumteka na wengine kumshambulia kwa maneno makali.

“Namna watu walivyokuwa wakinishambulia kwenye mitandao ya kijamii nilijisikia vibaya, hata msanii mwenyewe alilalamika sana na kuona kama nimehoji watu kumchafua, kiukweli nilijisikia vibaya,”

“Lakini kilichozungumzwa kwangu niliona ni kitu cha kawaida. Yale maneno na lawama vilinifanya nitafakari sana na mwisho wa siku nilijikuta nakata tamaa na nilitaka kuacha hii kazi,”anasema.

Anasema hali hiyo ilimuathiri kwa kiasi kikubwa kwasababu alipoteza uaminifu kwa baadhi ya watu maarufu, walikuwa wanahisi anafanya habari za uchonganishi na wengine alikuwa akitaka kuwahoji wanamuogopa kwa maswali yake au wakati mwingine wakimpa tahadhari na kumuomba asiandike baadhi ya mambo.

Anasema kuna baadhi ya wasanii hawana uelewa na vyombo vya Habari hivyo, amekuwa akizungumza kuwaelimisha kwa wale wanaomuogopa na mwisho wa siku wanamuelewa.

Roja licha kutengeneza uadui na staa huyo walisamehana na hadi Leo akikutana naye anamuhoji na hakuna chochote kibaya tena kinachotafsiriwa kwasababu kila mmoja alifahamu mapungufu yake na kurekebishana

Anasema taarifa yake hiyo iliyompa vitisho ilimpa funzo kubwa sana kwamba anapofanya kazi na watu hasa mastaa anahitaji kuwa makini kwasababu kuna vyanzo vingine vya habari vinaongea kulingana na atakavyoamka.

Wengine wanaweza kuamka vibaya wanapohojiwa huzungumza mambo mabaya ambayo yanaweza kuleta ugomvi upande wa pili.

Anawahimiza waandishi wa habari chipukizi kuwa makini, kuwa wavumilivu lakini pia, kujifunza kufanya uchunguzi wa kile wanachoenda kukihoji ili wapate taarifa sahihi za pande mbili bila kupendelea.