Mfanyabiashara ajinyonga, mwanachuo afa stendi

WATU wawili wamefariki katika matukio mawili tofauti akiwamo akiwemo mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Jordan aliyefia katika Kituo cha Mabasi Msamvu mjini Morogoro.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama Kamanda Mkama alisema tukio hilo la aliyefia kituoni, ni la usiku wa kuamkia Machi 2, na mwanafunzi huyo ni Magnos Timoth (22) mkazi wa Kipera ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Jordan.

Alisema Timoth alizidiwa ghafla na kujilaza chini mbele ya dada yake, Anna Mbonde (42) wakiwa wanasubiri usafiri wa basi kwenda Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma.

Kamanda Mkama alisema gari la polisi lilijitahidi kumuwahisha Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro lakini ilibainika alikuwa amefariki dunia.

Alisema uchunguzi wa awali uliofanywa na polisi ulionesha Timoth alikuwa akisumbuliwa na maradhi na alikuwa katika mpango wa kutafutiwa matibabu.

Katika tukio jingine, kamanda alisema mfanyabiashara na mkazi wa kata ya Lukobe, Nungu Nassoro (25) alikutwa amekufa kwa kujinyonga kwa kamba ya katani kwenye mti wa mwembe uliopo kwenye makazi yake.

Kamanda Mkama alisema Nassoro alijinyonga Machi Mosi, katika Mtaa wa Lukobe Manispaa ya Morogoro na chanzo kikitajwa kuwa ni msongo wa mawazo uliotokana na ugumu wa maisha.

Alisema baada ya uchunguzi mwili wa marehemu ulikabidhiwa kwa ndugu kwa taratibu za mazishi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button