Mfuko wa jimbo wafungua barabara Ilemela

JUMLA ya kilometa 126 za mtandao wa barabara zinazounganisha baadhi ya kata na wilaya zimefunguliwa kupitia fedha za mfuko wa jimbo chini ya usimamizi wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini TARURA Wilaya ya Ilemela

Akizungumza wakati wa zoezi la ufunguaji na uunganishaji wa mtandao wa barabara hizo katika barabara inayotoka Buswelu Mbogamboga kupitia Nyamadoke kuelekea Nyamhongolo,Mratibu wa barabara kutoka Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Ilemela, Dk Angeline Mabula, Mpunzi Mbegeje amesema kuwa ufunguaji na uunganishaji wa mtandao huo wa barabara utasaidia wananchi wa jimbo hilo.

”Mbunge anatambua changamoto za usafiri zinazowakabili wananchi wake hasa kipindi hiki cha mvua zilizokuwa zikinyesha, Lakini pia huu ni utekelezaji wa kile alichowaahidi wananchi wake wakati anawaomba kura katika uchaguzi Mkuu uliopita hivyo hiki anachokifanya ni utekelezaji wa ahadi zake pia ni uwekezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi” Alisema

Aidha Mpunzi ameiomba Serikali kuongeza bajeti ya fedha za mfuko wa Jimbo na bajeti ya wakala wa barabara za mijini na vijijini TARURA wilaya ya Ilemela ili kukidhi mahitaji ya wananchi ukilinganisha na uhitaji kwa kuwa wilaya hiyo imekuwa ikikua kwa kasi siku hadi siku jambo linalosababisha wakati mwingine kumlazimu Mbunge wa Jimbo hilo kutoa fedha zake binafsi mfukoni au kushirikiana na wadau wa maendeleo kwaajili ya ujenzi na ukarabati wa barabara na miundombinu mingine katika jimbo lake.

Kwa upande wake msimamizi wa ufunguzi wa mtandao huo wa barabara kutoka  TARURA Wilaya ya Ilemela Mhandisi Said Tano Irema mbali na kumpongeza mbunge wa Jimbo hilo Kwa namna anavyopambana katika kuomba Serikali kutekeleza miradi ya barabara ndani ya Jimbo lake amesema kuwa ofisi yake imeshapokea barabara 47 zilizofunguliwa na Mbunge huyo kwaajili ya kuzihudumia kama mamlaka ya usimamizi wa barabara za  ndani ya wilaya hiyo sanjari na kuishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hasan kwa fedha inazoleta katika kutekeleza miradi ya barabara .

Rubanila Matoforo Rubanila ni dereva wa bodaboda kutoka Kata ya Kahama eneo la Isela ambapo ameishukuru Serikali kwa ukarabati wa barabara ya kutoka Kahama senta kuelekea Isela itakayosaidia kuwainua kiuchumi kwa kurahisisha usafiri wa bidhaa na huduma kutoka Makazi yao kuelekea soko kuu la Buswelu huku Amina Songe akimpongeza Mbunge wa Ilemela kufuatia changamoto ya usafiri iliyokuwa ikiwakabili hasa kwa kina mama wajawazito wakati wa kujifingua wakitokea eneo la Isela kuelekea Zahanati ya Kahama.

Habari Zifananazo

Back to top button