Mgeja: Ni mkutano muhimu kwa CCM

DAR ES SALAAM;  MWANASIASA  aliyepata kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, amesema Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM utakaofanyika wikiendi hii ni mkutano muhimu kwa chama hicho, hivyo kuwatakia kila la heri wajumbe.

Akizungumza leo Januari 16, 2025 jijini Dar es Salaam, amesema kuwa shauku kubwa ya wana-CCM ni kumpata Makamu Mwenyekiti atakayemsaidia mwenyekiti wa chama ambaye ni Rais Samia Suluhu Hassan.

“Nina imani kuwa atapatikana Makamu Mwenyekiti atakayemsaidia Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Samia kwani CCM ina hazina kubwa ya viongozi na wenye uwezo wa kuongoza katika nyanja mbalimbali,” amesema Mgeja.

Amesema kuwa shauku kubwa ya Watanzania ni kuona nafasi ya Makamu Mwenyekiti ambaye atarithi mikoba ya Abdulrahman Kinana aliyeamua kupumzika, hivyo kiongozi huyo atakayechaguliwa atatimiza majukumu yake mapya kwa ushirikiano wa wana-CCM.

“Tunaamini kuwa atakayepatikana atakuwa ni mwenye kumshauri Mwenyekiti wa CCM Rais Samia katika kuleta mabadiliko ndani ya chama hivyo ni vyema sasa tukasubiri Mkutano Mkuu wa CCM unaotarajiwa kufanyika Januari 18 na 19, 2025, jijini Dodoma,” amesema Mgeja.

 

Habari Zifananazo

Back to top button