Mgogoro wamalizwa kampuni uchimbaji madini

KAMATI maalumu ya wataalamu wa ramani mgodini kutoka Chuo Cha Madini Dodoma imemamliza mgogoro kati ya Kampuni ya Franone na Gem & Rock Venture.

Afisa Mfawidhi wa Wizara ya Madini Mkoani Manyara, Mernad Msengi amesema madini kilo 4 yalichimbwa mita 650 ndani ya Mgodi wa Kitalu C unaomilikiwa na serikali na mwekezaji Mzawa Onesmo Mbise ni kinyume na sheria ya madini.

Mbali ya hilo Kamati imebaini katika uchunguzi wake kuwa mageti yaliyowekwa na Kampuni ya Gem & Rock Venture inayochimba mgodi kitalu B inayomilikiwa na Mkurugenzi Joel Mollel maarufu kwa jina la Saitoti yaliwekwa ndani ya Mgodi wa kitalu C eneo ambalo kampuni ya Saitoti inafanya uzalishaji.

Mernad Msengi amesema kuwa kuwa baada ya kamati kubaini hilo, iliagiza Kampuni ya Gem & Rock Venture kuwa mageti waliyowekwa chini ya ardhi yafuate leseni husika na Madini yaliyozalishwa katika eneo la mgogoro yataendelea kushikiliwa na serikali hadi hapo vinginevyo.

Msengi alisema majibu ya kusudio la kufungiwa mgodi iliyotolewa na Kampuni ya Gem & Rock Venture kwa Wizara ya Madini hayakuiridhisha ofisi yake hivyo mgodi utaendelea kusimamisha shughuli za uchimbaji hadi pale itakaporekebisha kwa ukamilifu makosa yote yaliyoelekezwa na Wizara ya Madini juu ya Ukiukwaji wa leseni uliofanywa na Kampuni hiyo.

Msengi alisema timu hiyo ya Wataalamu ilifanya kazi kwa muda wote ndani ya mgodi kushirikiana na vyombo vyote vya dola katika Wilaya ya Simanjiro{Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Simanjiro}, Viongozi wa Mgodi wa Kitalu C na B na baadhi ya Maofisa wa Wizara ya Madini lengo ni kutaka taarifa za kiuchunguzi ziwe wazi na huru na kusiwe na kificho ili kuondoa lawama zisizokuwa za Msingi kwa pande zote

Mbali ya Saitoti kumiliki Kampuni ya Gem & Rock Venture kwa kushirikiana na mkurugenzi mwenza, Sammy Mollel katika Mgodi Kitalu B walituhumiwa kuchimba Bomu katika Mgodi wa Kitalu C mgodi unamilikiwa na serikali na Mwekezaji Mbise maarufu kwa jina la Onee na kufanikiwa kutoweka na madini kilo 4 lakini kabla ya kukimbia nayo  Maofisa wa Wizara ya Madini Mirerani walifanikiwa kuwapora na kuyahifadhi katika ofisi Madini Mirerani.

Rais Dk Samia Suluhu Hassan aliwahi kusema katika hotuba zake siku za nyuma kuwa wale wote wanaochimba Bomu katika mgodi wa Tanzanite Kitalu C kuacha mara moja vinginevyo dola haitawaacha salama pindi watakapokaidi amri kwani kitalu C ni mali ya serikali na Mwekezaji Mzawa anayemiliki Kampuni ya Uchimbaji ya Franone ya Jijini Arusha

Hivi karibuni ilidaiwa kuwa wafanyakazi 30 wa Kampuni ya Gem & Rock Venture walivamia mgodi wa Kitalu C kwa njia ya Bomu na kuchimba Madini ya Tanzanite kibabe ndani ya mgodi huo na kufanikiwa kupora Madini ya kilo 4 hayo lakini uongozi wa Kampuni Ya Saitoti  ulipinga na kusema kuwa wao ndio wameporwa Madini ya Tanzanite yenye uzito wa kilo 6.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x