Mhandisi Masauni amjulia hali Waziri Mkuu Mstaafu Pinda

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amemtembelea na kumjulia hali, Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Peter Pinda nyumbani kwake Dodoma, leo Februari 10, 2026.

Mhandisi Masauni ameeleza nia ya ziara hiyo ni kumjulia hali, kupata uzoefu na ushauri namna bora ya kushughulikia masuala ya Mazingira na Muungano.

Akizungumza, Pinda ameshukuru ujio huo na akisema ni hekima na busara kupata mawili matatu kutoka kwa wastaafu.

Suala la Mazingira ni suala muhimu sana na ndio maana viongozi wa awamu zote sita wamekuwa wakilitilia maanani suala hilo.

Hivyo elimu kuhusu masuala ya Muungano na Uhifadhi wa Mazingira inapaswa kutolewa zaidi hasa kwa kundi la vijana ambao wengi wao bado hawana uelewa kwenye mambo hayo.

Aidha Waziri Mkuu Mstaafu Pinda ameongeza kuwa ni muhimu Biashara ya Kaboni nayo ikasimamiwa vyema kwani kwa kufanya hivyo itanufaisha jamii na kuongeza pato la taifa endapo watu wataelewa zaidi kuhusu biashara hiyo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button