Morris afikia tamati Azam

MATAJIRI wa Chamazi Azam FC wametangaza kufikia ukomo na Kocha wake msaidizi Agrey Moris Ambros aliyehudumu klabuni hapo tangu 2009 akiwa mchezaji kijana, nahodha na pia sehemu ya benchi la ufundi.

Taarifa hiyo imetolewa leo Juni 17, 2023 kupitia akaunti rasmi ya Instagram ya Klabu hiyo huku ikitoa shukurani kwa Ambros kwa muda wote aliyehudumu klabuni humo.

“Daima utabakia kwenye historia ya klabu yetu. Tunakutakia kila la kheri kwenye maisha yako mapya. You area a truelegend Agrey Moris Ambros. ”

Advertisement

Itakumbukwa mwanzoni mwa Juma Azam walitangaza kuachana na wachezaji kama nahodha Bruce Kangwa, Rogers Kolla, Ismail Aziz Kader, Daniel Amoah sambamba na Kocha wa walinda lango Dani Cadena bila kusahau aliyekuwa Kaimu Kocha Mkuu wa klabu hiyo Kalimangonga Ongala .

Huu ni muendelezo wa panga pangua ya safu ya Azam FC na vilabu vingine nchini ikiwa ni maandalizi ya msimu ujao 2023/24 ambapo msimu uliotamatika mwezi jana Azam FC walimaliza wakiwa nafasi ya tatu huku wakikusanya alama 59 katika michezo 30 ya NBCPL sambamba na kumaliza nafasi ya pili ya Kombe la Shirikisho Azam baada ya kufungwa 1-0 katika mchezo wa fainali dhidi ya Yanga.

/* */