Miaka 60 Msondo Ngoma kufanyika Chang’ombe

TAMASHA la miaka 60 ya Msondo Ngoma Music Band Baba ya muziki wa Dansi linatarajia kufanyika Oktoba 26 mwaka huu katika viwanja vya Gwambina Lounge zamani TCC Club Changombe jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Meneja wa bendi ya Msondo Ngoma, Saidi Kibiriti, amesema kuwa bendi hiyo itaweka kambi ya wiki mbili mkoani Dodoma kwa nia ya kujifua zaidi.

Advertisement

“Msondo ngoma tuna jambo letu la Miaka 60 kuanzishwa tamasha la sasa litakuwa na vitu vizuri na ubunifu ndani ya miaka 10 iliyopita baada ya kuadhimisha miaka 60 wamejiunga wanamuziki wengi.”

“Miaka 60 ya Msondo Ngoma Bendi itaanza na kisomo kitakachofanyika Oktoba 13 Hamana ofisini za bendi hiyo ikiwa ni sehemu ya kuwakumbuka waimbaji waliotangulia mbele za haki,”

“Waimbaji wanafanya mazoezi ya kutosha siku hiyo wataimba ‘live’ ili kukonga nyoyo za mashabiki zao wanaoipenda Msondo Ngoma wakati wote wanapotoa burudani,”amesema Kibiriti.

Kwa upande wake msanii Freshi Jumbe anayeishi nchini Japan aliyetamba na wimbo wa ‘penzi ni kikoozi amesema kuwa ni miongoni mwa waimbaji wa bendi ya Msondo na ameimba nyimbo nyingi atazifanyia mazoezi na ataimba siku hiyo.

Ally Choki amesema kuwa siku hiyo ataimba wimbo alioimba na Mzee Ngurumo Baba ulichomtendea Mama pamoja na husia wa wazazi.