“Michezo muhimu kwa afya”

MOROGORO: WANAMICHEZO 636 kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania na taasisi nyingine zinazohusiana na bandari wameshiriki michezo mbalimbali (Interports Games),kwa ajili ya kuimarisha afya na kufanikisha kuleta ufanisi wenye tija kazini.
Mwenyekiti wa Kamati ya Rasilimali Watu ya Bodi ya Wakurugenzi wa TPA,Mhandisi Abdallah Mwinyi,amesema hayo kabla ya kumkaribisha mkuu wa wilaya ya Morogoro, Mussa Kilakala kufungua michezo ya 18 ya Bandari ‘INTER-PORTS GAMES’ 2025 katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Amesema wanamichezo hao kati yao, 466 ni kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), 95 kutoka Shirika la Bandari Zanzibar (ZPC),52 kutoka Kampuni ya DP WORLD Dar es Salaam na 23 kutoka Kampuni ya Meli Tanzania (TASHICO).
Mhandisi Mwinyi aliitaja michezo itakayofanyika kwa muda wa siku tano imehusisha mpira wa miguu, Netiboli ,Basketball, Volleyball, riadha , kuvuta kamba na michezo ya jadi ikiwemo ya bao , karata na draft.

“Mchezo ambao haupo ni ngumi ingawa miaka ya nyuma ulikuwa una maarufu wa kipekee kwa TPA baada ya soka , ulifikia siku za nyuma mabondia wa Mamkala walishiriki vyema hadi kwenye mapambano ya kitaifa nah ii ni changamoto kwa Mamkala kuurejesha mchezo huu siku zijao,” amesema Mhandisi Mwinyi.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Michezo hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala, Mbarikiwa Masinga amesisitiza kuwa mamlaka hiyo inatambua nafasi muhimu ya michezo kwa wafanyakazi wake, si tu kwa afya, bali pia kwa ufanisi kazini.
Masinga amesemamichezo hiyo pia ni jukwaa la kuibua vipaji na kuimarisha uhusiano wa kikazi miongoni mwa wafanyakazi kutoka vitengo mbalimbali na wa mikoa mbalimbali yenye bandari
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mussa Kilakala,akifungua michezo huo amewataka wakati wa kushindana waitumie kuongeza mahusiano mema na ushindi wa kila timu iwe ni ishara ya kutaka kuzalisha kwa tija zaidi katika maeneo yao ya kazi.
“Tutumie michezo hii kama sehemu ya kampeni ya kuimarisha afya zetu na kubwa zaidi kuongeza tija na ufanisi pamoja na kuleta mshikamano kwa Wafanyakazi “ alisema Kilakala .
Mkuu huyo wa wilaya amewataka baada ya kurudi kwenye vituo vyao vya kazi wanapaswa kujituma zaidi, umakini na uadilifu na ufanisi mkubwa ili kuongeza tija
Michezo ya 18 ya Bandari ‘inter-ports games’ imebeba kauli mbiu: “Michezo ya Bandari 2025 kwa afya, tija na mshikamano kwa wafanyakazi; tujitokeze kupiga kura Oktoba 29” .




Freedom to work whenever I want — that’s what I love! I made $18,542 in a month doing this online. Check the details ———————⊃⫸ https://dailycash21.blogspot.com/