TANGA; Handeni. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Dk Stergomena Tax amesema serikali inatarajia kukamilisha ujenzi wa nyumba 5,000 ambazo zimeanza kujengwa za wakazi wa Msomera wilayani Handeni mMkoa wa Tanga waliohama kwa hiari kutoka Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro ndani ya miezi sita kutoka sasa.
–
Dk Tax ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kutembelea kuona maendeleo ya ujenzi wa nyumba hizo zinazojengwa katika Kijiji cha Msomera mkoani Tanga, akiongozana na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Geophrey Pinda.
–
“Lengo letu ni kuhakikisha kwamba nyumba 1,000 zinakamilika mwishoni mwa mwezi Oktoba 2023 na tutaendelea kuzikabidhi nyumba kadri zinavyokwisha, lakini nyumba 5,000 zinarajiwa kukamilishwa mwishoni mwa mwezi Machi 2024,” amesema.
Kama mnavyoona hii ni oparesheni inayofanywa na Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) hususan Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ambapo ujenzi huu unahusisha sekta nyingi na ndio maana nimeongozana na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleeo ya Makazi na sekta nyingine za Nishati na Maji ili kufanya haraka kwa wakazi hawa kupata Malazi ya kudumu” Aliongeza Dk. Tax.
Naye Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Geophrey Pinda amesema Wizara yake ndio ya mwanzo kabisa katika utekelezaji wa mradi huu kwani ndio inafanya maandalizi ya kupanga na kupima ardhi ili sekta nyingine zianze kufanya kazi kikamilifu.
“Wizara yetu ndio ya kwanza kabisa kufika eneo hili kuja ambapo ilikuja kulitambua eneo hili la msomera tangu lilipotolewa agizo la kuwaandalia makazi wananchi wa eneo hili, hivyo tumefanikiwa kulipanga na kulipima japo bado baadhi ya maeneo tunaendelea kuyapanga na kutatua migogoro ya mipaka” Alisema Pinda.
Comments are closed.