Miili 19 ya marehemu ajali ya Precision air kuagwa leo

Miili ya marehemu ajali ya Precision air

MIILI 19 ya marehemu wa ajali ya ndege ya Precision Air imewasili katika uwanja wa Kaitaba Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera kwa ajili kuagwa, zoezi linalotarajiwa kuongozwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Watu 19 kati ya 43 waliokuwa wakisafiri kutoka Dar es Salaam Jumapili walipata ajali na kufariki Dunia baada ya ndege kushindwa kutua katika uwanja wa ndege wa Bukoba mjini kutokana na hali mbaya ya hewa na kuanguka katika Ziwa Victoria.

Baadhi ya ndugu wa marehemu, viongozi wa Dini na Serikali pamoja na wananchi pia wamefika katika uwanja wa Kaitaba ili kutoa heshima zao za mwisho kwa wapendwa wao.

Advertisement

Wafanyakazi watano kati ya nane wa Shirika la Menejimenti na Maendeleo ya Afya (MDH) waliokuwa wakisafiri kwa ndege hiyo walifariki Dunia. Wengine ni Rubani wa ndege hiyo, Burundi Lubaga na Msaidizi wake Peter Odhiambo pamoja na ndugu wawili wa familia moja.

/* */