Mikoa yajipanga kuimarisha amani, umoja

BAADHI ya wakuu wa mikoa wamebainisha mikakati ya kuhakikisha maeneo yao na wananchi yanaendelea kuwa na amani na kuendelea kufanya shughuli zao za kijamii na kiuchumi kama kawaida.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa mafuta na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), amesema hali ya usalama katika mkoa huo ni shwari na wananchi wote wanaendelea na shughuli zao za kijamii na kiuchumi kama ilivyokuwa hapo awali na huduma zote zinapatikana kwa wakati.

Amesema miongoni mwa mikakati ya mkoa huo katika kuendelea kuhakikisha usalama na amani inatawala ni ku- hakikisha vyombo vyote vya ulinzi na usalama vinaendelea kutimiza majukumu yake kwa mujibu wa sheria.

SOMA: Maisha yarejea kawaida, serikali yapongezwa

Chalamila amefafanua kuwa wamepanga kukutana na makundi yote ya jamii kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya taifa na changamoto walizonazo pamoja na kupokea ushauri ili kujenga taifa moja na kudumisha amani kwa mujibu wa maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan.

“Hivi sasa, jeshi la polisi linaendelea kufanya uchunguzi kuhusu watu waliokuwa wakifanya vurugu hizo na kuhakikisha wote waliohusika wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria,” amesema Chalamila.

Amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya serikali,vyombo vya usalama, wadau na wananchi wote katika kulinda amani na umoja wa taifa.

“Hatutaki kuona mtu yeyote akipoteza maisha. Madhara yanayoweza kump- ata mtu asiyehusika siyo dhamira ya Jeshi la Polisi, lengo letu ni kulinda amani na usalama wa kila Mtanzania na taifa kwa ujumla.

Tuendelee kuwa wavumilivu na kushikamana, taifa letu ni moja na lazima libaki kuwa moja,” amesema.

Aidha, aliwataka viongozi wa serikali za mitaa kushirikiana na watendaji kutoa elimu kwa vijana wa boda- boda, bajaji na wamachinga juu ya madhara ya vurugu na umuhimu wa kulinda amani.

“Huu ni wakati wa uponyaji. Kila mmoja azung- umze, tuchambue masuala yanayohitaji utekelezaji wa haraka na yale yanayohitaji mchakato wa kisheria. Tanzania ni moja, haigawanyiki,” amesisitiza.

Chalamila alitoa wito kwa wakazi wa Dar es Salaam kudumisha amani na utulivu, akisisitiza kwamba mkoa huo ni chachu ya uchumiwa taifa, hivyo vurugu au uharibifu wowote huathiri uchumi na maisha ya Watanzania wengi.

Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka amesema serikali na uongozi wa mkoa huo utaendelea kuhakikisha wakazi wa Njombe wanasikilizwa na wanapata haki wanazostahili ili kujenga mkoa na kuinua uchumi wa watu wa mkoa huo.

Ametoa pole kwa wananchi waliopoteza ndugu zao na kuwahakikishia kuwa usalama na amani utaendelea kutawala kwa sababu Jeshi la Polisi limeendelea kuhakikisha wananchi wanakuwa salama. Aidha, aliwasihi wakazi wa mkoa huo kuon- doa hofu na waendelee na shughuli zao za kijamii.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Amos Makalla amesema hali ya usalama ni shwari na wanatekeleza maelekezo ya Rais Samia ya kwamba mkoa huo ni mkoa wa kibiashara na kiutalii kuhakikisha wageni wote wanapata huduma zote za msingi walizojia, ikiwemo utalii na wanaondoka salama.

“Tunawahakikishia wananchi wa Arusha kwamba vyombo vya ulinzi na usalama vitaendelea kuhakikishaia usalama wao na vyombo vya ulinzi wanavyoviona vinafanya doria ni kwa ajili ya kuhakikisha wananchi wanakuwa salama, hivyo watoe ushirikiano ili mkoa wetu uendelee kuwa salama,” amesema Makalla.

Pia, alisema amewaagiza wenyeviti wa serikali za mitaa kutoa ushirikiano katika kutoa taarifa za usalama kati- ka vyombo vya usalama pale wanapoona kuna viasharia vya uvunjifu wa amani.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda amesema usalama umerejea kwa asilimia 100 na wanaendelea kuhakikisha usalama unakuwepo muda wote kwa kutoa maagizo kwa Jeshi la Polisi na vyombo vyote vya usalama kuhakikisha mkoa huo unasalia kuwa salama.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amesema kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wameendelea kuwatoa hofu wananchi ili waendelee kufanya shughuli zao kwa amani na utulivu.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button