Chalamila asisitiza amani Dar

DAR ES SALAAM: MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amekutana na wadau wa Nishati ya Mafuta katika kikao maalumu Da es Salaam.

RC Chalamila ameongoza mjadala wa ulinzi na usalama wa vituo vya kuuzia mafuta kufuatia vurugu zilizoibuka hivi karibuni na kupelekea baadhi ya vituo kuchomwa moto.

Aidha, Chalamila amewapa pole wadau hao na kuendelea kuwatia moyo kuwa Serikali bado iko bega kwa bega na wafanyabiashara hao kwa kuwa wana mchango mkubwa katika mnyororo wa uchumi wa mtu mmoja mmoja lakini pia taifa kwa ujumla.

“Ni vema sasa kuratibu vizuri uuzwaji wa mafuta kwenye vidumu, kwa kuwa huwezi kuzuia kabisa kwa kuwa yako maeneo au vyombo vinavyotumia nishati hiyo huitaji mafuta yapelekwe kama vile minara ya simu na boti,” alisema Chalamila.

Pia amewataka wadau na jamii kwa ujumla kuendelea kutoa elimu kwa vijana hususani katika makundi yao kama vile pikipiki, na bajaji kutambua umuhimu wa kulinda na kudumisha amani katika mkoa huo kwa kuwa Dar es Salaam inahudumia nchi nyingi zisizo na bandari pamoja na kuwepo kwa shughuli nyingi za kujipatia kipato na huduma za afya za kibingwa.

Mwisho wadau hao wameishukuru Serikali na kuiomba kuongea na mabenki ambayo walikopa fedha kuwapa muda kidogo wa kuweza kujipanga kurejesha mikopo hiyo.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo ametoa rai kwa wafanyabiasha hao kuongeza ulinzi lakini pia katika vituo vya mafuta pasiwe na biashara tena zingine ili kujihakikishia usalama zaidi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button