Serikali yaanza kutoa mikopo mfuko wa maendeleo ya vijana

ARUSHA; SERIKALI imeanza rasmi kutoa mikopo kupitia Programu ya Sh bilioni 200 chini ya Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, huku Mkoa wa Arusha ukiwa wa kwanza kunufaika kwa kupokea Sh milioni 730 ambayo ni sehemu ya utekelezaji wa awamu ya kwanza ya mpango.
Mpango wa awamu ya kwanza unalenga kuwawezesha vijana kujiajiri na kukuza shughuli za uzalishaji mali.
Uzinduzi wa utoaji wa mikopo hiyo umefanyika jijini Arusha, ambapo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka, amesema serikali imepokea maombi 30,384 kutoka kwa vijana wa maeneo mbalimbali nchini.

Katika uzinduzi huo, Mkoa wa Arusha umepokea mikopo yenye thamani ya Sh milioni 730 kwa miradi mitatu ya vijana, kati ya fedha hizo, Sh million in 500 zimetengwa kwa ajili ya mradi wa utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu.
Amesema Sh milioni 130 zimetengwa kwa ajili ya kiwanda cha vijana kinachozalisha chaki zisizotoa vumbi, huku Sh100 milioni zikitolewa kwa vikundi vya mama na baba lishe ili kuongeza uwezo wao wa uzalishaji na biashara, kuanzisha na kuendeleza shughuli za uzalishaji mali.

Naye, Meneja wa Benki ya CRDB, Tawi la Meru, Haika Mawalla, amesema benki hiyo imejipanga kuhakikisha utekelezaji wa mpango wa mikopo yenye masharti nafuu kwa vijana unafanyika kwa uwazi, ufanisi na uwajibikaji ili kuwafikia walengwa wengi zaidi nchini.
Amesema mbali na kutoa mikopo, benki hiyo itaendelea kuwajengea vijana uwezo kupitia elimu ya fedha, usimamizi wa biashara na matumizi sahihi ya mikopo.
“Tunaamini kuwa mchanganyiko wa mtaji, maarifa na nidhamu ya fedha ndiyo msingi wa mafanikio ya biashara na ujasiriamali endelevu. Tunawasihi vijana wote kuitumia fursa hii kwa ubunifu na uwajibikaji ili mikopo hii iwe chachu ya kuongeza uzalishaji, ajira na ukuaji wa



