Mikopo ya halmashauri yawa kichocheo ajira kwa vijana

KIGOMA: SERIKALI imesema mikopo inayotolewa kutoka kwenye mapato ya ndani ya halmashauri za Mkoa Kigoma imekuwa chachu katika kutengeneza ajira kwa vijana, kuchochea uchumi na biashara kwa wakazi wa mkoa huo.

Katibu Tawala wa Wilaya Kigoma, Mganwa Nzota shayo amesema hayo wakati akizungumza katika hafla ya kukibidhi pikipiki sita kwa vikundi viwili vya vijana na wanawake zenye thamani ya Sh milioni 21 mikopo iliyotolewa kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kupitia Benki ya CRDB katika mpango wa Imbeju.

Katibu Tawala wa Wilaya Kigoma, Mganwa Nzota akizungumza katika hafla ya kukibidhi jumla ya pikipiki sita kwa vikundi viwili vya vijana na wanawake zenye thamani ya shilingi milioni 21 mikopo iliyotolewa kupitia mapato ya ndani ya Hamashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Nzota amesema kutokana na umuhimu vijana katika kuchochea shughuli za kiuchumi serikali imeweka mkazo kwa halmashauri kuhakikisha inatenga fedha na kutoa mikopo kwa vijana kuanzisha na kuendeleza shughuli zao za kiuchumi lakini pia shughuli wanazoanzisha kuwa chachu katika kuajiri vijana wengi Zaidi.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Anselm Mwenda amesema kumekuwa na mafanikio makubwa kwa vijana kuona umuhimu wa mikopo hiyo na hivyo wengi kujitokeza na kwamba hadi sasa tangu mpango huo kuanza jumla ya maombi 855 yamepokelewa kutoka kwa vikundi vya vijana, wanawake, na walemavu kwa Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Katibu Tawala wa Wilaya Kigoma Mganwa Nzota (kushoto) akikabidhi funguo na kibao cha namba kama ishara ya kukabidhi pikipiki kwa viongozi wa vikundi vya vijana na wanawake vya Manispaa ya Kigoma ambao wamekuwa wanufaika wa mikopo ya pikipiki kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma

Awali Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma, Jabiri Majira alisema kuwa kwa mwaka huu wa fedha hadi sasa kiasi cha Sh milioni 619 zimeshatolewa mikopo kwa vikundi 66 kati yao vikundi vya vijana 15, wanawake 47 na walemavu vikundi vinne.

Anselm Mwenda Kaimu Meneja CRDB Kanda ya Magharibi

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button