Mila, desturi zatajwa kuwa muhimu kwa maendeleo

KIGOMA: JAMII mkoani Kigoma imetakiwa kuendelea kuwafundisha vijana mila, utamaduni na desturi za jamii husika kama njia ya kuchochea maendeleo na utu kwa jamii ili kuwafanya vijana kuishi kwenye maadili mema.

Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma, Aida Nzowa alisema hayo wakati wa ibaada ya kiasili ijulikanayo kama Elombe inayoratibiwa na shirika lisilo lalkiserikali la maendeleo ya kijamii katika asili na tamaduni (SHIMKIATA) ambayo huwakutanisha watu kutoka maeneo mbalimbali duniani.

Nzowa alisema kuwa ibaada za namna hiyo ni muhimu kuendelea kuenziwa kwani inasaidia jamii kurudi kwenye misingi ya upendo na mshikamano na kusaidia watu kutofanyiana mambo mabaya sambamba na kusaidia vijana kujengwa kwenye makuzi ya kuheshimu watu kubwa na kuwa na nidhamu na maadili katika malezi yao.

Akizungumza katika ibada hiyo ya Ilombee, Kiongozi wa wanajadi duniani kwa bara la Afrika Mwami Lokoko amesema jadi ina muhimu katika kuwasaidia watu kutambua chimbuko lao na misingi ya kale ikiwemo kutambua misingi ya kiroho.

Mwami Lokoko alisema kuwa wataendelea kufundisha kueleza umma ili uweze kufahamu na kutambua asili na jadi yao ilivyo ili iweze kuwasaidia kuishi katika misingi ya kusaidiana na kutokengeuka na kuhadaliwa na ulimwengu wa sasa na kufanya mambo ya hovyo ambayo ni kinyume na mila na desturi zetu.

Ibaada hiyo imeenda sambamba na utoaji wa misaada kwa wasiojiweza, kufungisha ndoa mbili za kimila ikiwa chini ya kaulimbiu isemayo “Elombe ni urithi wetu, Amani yetu, Umoja wetu, Faraja kwa wenzetu kwa maendeleo endelevu.

Habari Zifananazo

4 Comments

  1. ᴄᴀꜱʜ ᴇᴀʀɴɪɴɢ ᴊᴏʙ ᴛᴏ ᴇᴀʀɴꜱ ᴍᴏʀᴇ ᴛʜᴀɴ $700 ᴘᴇʀ ᴅᴀʏ. ɢᴇᴛᴛɪɴɢ ᴘᴀɪᴅ ᴡᴇᴇᴋʟʏ ᴍᴏʀᴇ ᴛʜᴀɴ $3500 ᴏʀ ᴍᴏʀᴇ ꜱɪᴍᴘʟʏ ᴅᴏɪɴɢ ᴇᴀꜱʏ ᴡᴏʀᴋ ᴏɴʟɪɴᴇ. ɴᴏ ꜱᴘᴇᴄɪᴀʟ ꜱᴋɪʟʟꜱ ʀᴇQᴜɪʀᴇᴅ ꜰᴏʀ ᴛʜɪꜱ ᴊᴏʙ ᴀɴᴅ ʀᴇɢᴜʟᴀʀ ᴇᴀʀɴɪɴɢ ꜰʀᴏᴍ ᴛʜɪꜱ ᴀʀᴇ ᴊᴜꜱᴛ ᴀᴡᴇꜱᴏᴍᴇ. ᴀʟʟ ʏᴏᴜ ɴᴇᴇᴅ ɪꜱ 2 ʜʀꜱ ᴀ ᴅᴀʏ ꜰᴏʀ ᴛʜɪꜱ ᴊᴏʙ ᴀɴᴅ ᴇᴀʀɴɪɴɢ ᴀʀᴇ ᴀᴡᴇꜱᴏᴍᴇ. ᴇᴠᴇʀʏ ᴘᴇʀꜱᴏɴ ᴄᴀɴ ɢᴇᴛ ᴛʜɪꜱ ʙʏ ꜰᴏʟʟᴏᴡ ᴅᴇᴛᴀɪʟꜱ ʜᴇʀᴇ…

    .

    ᴍᴏʀᴇ ᴅᴇᴛᴀɪʟꜱ ꜰᴏʀ ᴜꜱ ————————➤ join.work43.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button