Milioni 322/- kujengea chanzo kipya cha maji Mkele

SERIKALI kupitia Wizara ya Maji imetoa Sh milioni 322 kujenga chanzo kipya cha maji cha Mkele ili kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji kwa wakazi wa mji wa Mbinga mkoani Ruvuma.

Kaimu Meneja wa Kitengo cha usambazaji maji wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa mazingira Mbinga mjini (Mbiuwasa), James Kida alisema chanzo hicho kina uwezo wa kuzalisha lita 50,000 kwa siku na ujenzi wake umekamilika.

Alisema walilazimika kujenga chanzo hicho kufidia upungufu wa maji uliotokana na utekelezaji wa mradi mpya wa maji wa Lusaka unaohudumia takribani watu wapatao 12,000 kutoka kata tatu za Ruhuwiko, Betherehemu na Matarawe.

Kida alitaja vyanzo vingine vinavyohudumia wananchi wa Mji wa Mbinga ni Ndengu kilichojengwa mwaka 1984 na vyanzo vinne vilivyopo Kijiji cha Tukuzi kwenye mlima maarufu wa Lupembe ambavyo vimejengwa mwaka 2018

Habari Zifananazo

Back to top button