Mipira 1,402 yasambazwa michezo mikoani

DAR ES SALAAM: SERIKALI kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imegawa jumla ya mipira 1,404 katika mikoa 26 ya Tanzania Bara kwa ajili ya mashindano mbalimbali ya michezo.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha 15 cha Maofisa Utamaduni na Maofisa Maendeleo ya Michezo wa Tanzania Bara. Kinachohudhuriwa na washiriki 900 kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Msigwa amesema kuwa ugawaji huo wa mipira ni matokeo ya utekelezaji wa maazimio ya vikao kazi vilivyopita, ambapo juhudi zinafanyika kuboresha sekta ya utamaduni, sanaa na michezo kwa ujumla.
Ameeleza kuwa lengo kuu la kikao kazi hicho ni kuleta mabadiliko chanya katika sekta hizo kwa kuandaa mikakati mipya, ikiwemo kuunganisha mifumo ya TAUS na AMIS, kuendeleza kampeni ya uzalendo wa kitaifa, pamoja na maandalizi ya medani za mbio ndefu za kimataifa kwa lugha ya Kiswahili zitakazofanyika mwaka 2025.
Aidha, katika kikao kazi hicho, maofisa watapata pia fursa ya kutembelea baadhi ya miundombinu ya michezo inayotarajiwa kutumika katika mashindano ya CHAN mwaka 2025 na AFCON mwaka 2027, ambayo Tanzania ni mwenyeji mwenza.
I’m getting 88 D0llars consistently to deal with net. Q I’ve never accepted like it tends to be reachable anyway one of my most noteworthy buddy got D0llars 27,000 D0llars in three weeks working this basic task and she impacted me to avail…
Take A Look Here….> http://Www.HighProfit1.Com